ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 31, 2020

LEO NI MIAKA 10 YA BLOG YA VIJIMAMBO

Image result for vijimambo blog logoImage result for vijimambo blog logo
Kwanza ni kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uwezo wake leo Vijimambo Blog yako pendwa imetimiza miaka 10 tangu ilipoanzishwa siku ya Jumapili, Januari 31, 2010 na kuzinduliwa rasmi na Mhe.Balozi Mwanaidi Maajar siku ya Jumamosi Octoba 23, 2010.

Pongezi nyingi kwa wadau wote USA na Duniani kwa ujumla, Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali, wadau wa habari ndani na nje ya Tanzania,

Historia yaVijimambo ni ndefu sana na katika historia hiyo huwezi kuwasahau Kalley Pandukizi aliyetia mkono wa mwanzo na kuelekeza njia ya blog ya Vijimambo itakapoelekea, Jojo aliyetengeneza sura na mwoenekano wa blog yako pendwa, Ebra NY, Rachel, Casius Mpambamaji  bila kusahau wote kwa ujumla wanao simama mstari wa mbele na kuhakikisha libeneke ya Blog ya Vijimmbo linasonga mbele..

Miaka 10 si kidogo Blog ya Vijimambo imepitia changamoto nyingi ikiwemo milima na mabonde, si kila kilichobandikwa humu kilimfurahisha kila mtu, na kama Blog yako ilikukosea kwa njia moja au nyingine tunaomba radhi kwani hilo halikua kusudio letu.

Tunamshukuru Mungu kwa kutujalia hapa tulipofikia zaidi atuangazie tuzidi kwenda mbali zaidi.

Timu ya Stars United ina mchngo mkubwa katika kuipaisha blog hii, shukurani nyingi sana kwenu, Bandio Mubelwa shukurani sana kwako. Kijiwe cha ughaibuni asante.

Mbarikiwe sana wadau wotewa Vijimambo USA na kote Duniani.

Vijimambo Timu.

No comments: