KLABU ya Yanga leo Jumamosi Feburuari 1, 2020 wamemshusha, Carraca Antonio Domingos Pinto raia wa Ureno kwaajili ya kusimamia mfumo wa uendeshaji wa klabu yao.
“Ukiangalia wasifu wake utaona kabisa kwamba huyu jamaa ni wa namna gani, alipita Benfica ambapo imewatoa wachezaji wengi pia amekuwa bora katika kuwauza wachezaji wao kama Contrao na wengineo,” alisema.
Yanga wapo katika mkakati wa kuelekea kwenye mabadiliko ya kiuendeshaji na wamemleta Domingos kwaajili ya kusaidia mchakato huo kuwa wa mafanikio.
Domingos aliwahi kufanya kazi na Benfica mwaka 2008-2013 akiwa Meneja Mkuu kabla ya baadae kutimkia kampuni ya WSPORTS 7 akiwa kama meneja mkuu. GPL



No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake