Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto) akimsalimia Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima, wakati alipokuwa anawasili ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam, leo. Simbachawene na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio waliwasili katika ofisi hiyo baada ya Katibu Mkuu kuapishwa Ikulu, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio akiongozwa na Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima (kulia), wakati alipokuwa anawasili ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam. Kadio aliwasili ofisini hapo baada ya kuapishwa Ikulu,jijini humo leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (kulia) akiwasalimia Watumishi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi wakati alipokuwa anawatembelea ofisini jijini Dar es Salaam. Kadio aliwasili ofisi ndogo ya Wizara jijini humo, baada ya kuapishwa Ikulu, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia) akimsalimia Mtumishi wa Wizara hiyo, Edaline Osima, ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam, leo. Simbachawene na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio waliwasili katika ofisi hiyo baada ya Katibu Mkuu huyo kuapishwa Ikulu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akimfafanulia jambo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio (kushoto), na Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima (kulia), katika kikao kilichofanyika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam, leo. Simbachawene na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio waliwasili katika ofisi hiyo baada ya Katibu Mkuu huyo kuapishwa Ikulu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (kulia), akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima, alipokuwa anamfafanulia jambo, mara baada ya Katibu Mkuu huyo kuwasili ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam, baada ya kuapishwa Ikulu, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Sheria na Hifadhi wa Idara ya Huduma ya Wakimbizi, Numbilya Mpolo, alipokua akitoa maelezo ya majukumu yake katika Idara hiyo. Kadio aliwasili ofisi ndogo ya Wizara hiyo jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuapishwa Ikulu, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (kulia) akiwasalimia Maafisa wa Idara ya Huduma ya Uangalizi na Probesheni wakati alipowatembelea ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam, leo. Kadio aliwasili katika ofisi hizo baada ya kuapishwa Ikulu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake