Mkurugenzi Idara ya uratibu wa shughuli za serikali SMT, SMZ Ndugu Khalid Bakari Amrani akiyafunga mafunzo ya siku mbili kwa watendaji wa taasisi za serikali juu ya uhakiki wa walengwa wa kaya Maskini katika ukumbi wa Suza Kampasi ya Nkurumah wakati.
Watendaji wa taasisi za serikali juu ya uhakiki wa walengwa wa kaya Maskini wakifuatilia Hotuba ya Ufungaji wa mafunzo yao uliofanywa na Mkurugenzi Idara ya uratibu wa shughuli za serikali SMT, SMZ Ndugu Khalid Bakari Amrani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {Tasaf } Nd. Ladislaus Mwamanga Kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Idara ya uratibu wa shughuli za serikali SMT, SMZ Ndugu Khalid Bakari Amrani mara baada ya mafunzo ya Watendaji wa taasisi za serikali juu ya uhakiki wa walengwa wa kaya Maskini ukumbi wa Suza Kampasi ya Nkurumah wakati.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Watendaji kutoka taasisi mbali mbali za serikali ya Mapinduzi wametakiwa kutekeleza vyema majumu yao watakayopewa katika zoezi la uhakiki wa taarifa za Wananchi wa Kaya maskini kwa kutunza siri za walengwa hao ili kuenda sambamba na maadili ya kazi zao.
Mkurugenzi Idara ya uratibu wa shughuli za serikali SMT, SMZ Ndugu Khalid Bakari Amrani ameleza hayo katika ukumbi wa Suza Kampasi ya Nkurumah wakati akiyafunga mafunzo ya siku mbili kwa watendaji wa taasisi za serikali juu ya uhakiki wa walengwa wa kaya Maskini.
Mkurugenzi Khalid amewaeleza watendaji hao kuwa taaria zote watakazokutana nazo zinazowahusu walengwa ikiwemo hali ya kipato na mambo mengineyo yanapaswa kuwa siri bila kuwekwa hadharani kwa mujibu ya taratibu na maadili ya ukusaji wa taarifa.
“Lakini napenda niwaeleze mtapokwenda huko taarifa za mtu yeyote ni siri kwa hivyo jambo la kwanza la kuzingitia ni uweka wa siri”
Amewataka wahusika hao wajitahidi kuwa makini katika suala zima la utumiaji wa lugha nzuri wakati wa kufanya mahojiano na walengwa ili kuepusha migogoro baina ya pande mbili hali itakayosaidia kulifanya zoezi kuwa rahisi na serikali kufikia lengo ililolikusudia.
Akizungumzia suala la uwasilishaji wa taarifa sahihi Mkurugenzi Khalid amewaomba wataendaji hao kutumia mbinu na utalamu waliyo nao katika kuhakikisha wanapata taarifa za kweli na sahihi ili kuondoa changamoto zilizojitokeza siku zilizopita kama vile kuwepo kwa kaya hewa.
Wakielezea lengo la kutolewa kwa mafunzo hao Mratibu wa TASAF Unguja Ndugu Makame Ali Hali na Mratibu wa TASAF Zanzibar Ndugu Saida Saleh Adam wamesema kufanyika kwa mafunzo hayo ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli lililowataka watendaji hao kabla ya kufanyika kwa zoezi la uingizaji wa fedha kwa walenga kufanyiwa kwa uhakiki.
Wamesema uhakiki huo utasaidia kufanya marekebisho ya taarifa pamoja na kutambua usahihi wa taarifa hizo kama zinakwenda sambamba na zile taarifa zilizokusanywa awali.
Wamefafanua kuwa zoezi hilo litafanyika kwa muda wa siku tatu kwa shehia mia moja ishirini sita kwa Unguja na Shehia 64 kwa upande wa kisiwa cha Pemba.
Mafunzo hayo yamekwenda sambamba kitendo cha kula kiapo kwa watendaji hao ili kuonyesha utayari wa kwenda kuitumiakia dhamana waliokabidhiwa.
No comments:
Post a Comment