BAADHI
ya waratibu wa uchaguzi wa mikoa,wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi
wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Jimbo wakisaini fomu za viapo katika
mafunzo ya siku tatu yanayoendelea shule ya Sekondari Galanosi Jijini
Tanga
Waratibu wa uchaguzi wa mikoa,wasimamizi wa uchaguzi na
wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Jimbo wakisaini fomu za viapo
katika mafunzo ya siku tatu yanayoendelea shule ya Sekondari Galanosi
Jijini Tanga
BAADHI ya waratibu wa uchaguzi wa mikoa,wasimamizi wa uchaguzi na
wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Jimbo wakisaini fomu za viapo
katika mafunzo ya siku tatu yanayoendelea shule ya Sekondari Galanosi
Jijini Tanga
TUME
ya Taifa ya uchaguzi NEC leo imeanza kutoa mafunzo ya siku tatu kwa
waratibu wa mikoa na wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kwa
mikoa ya Tanga na Kilimanjaro yenye lengo la kuwajengea uwezo wsatendaji
hao ili waweze kutekeleza majuku yao kwa ufanisi katika uchaguzi mkuu
Octoba 28 mwaka huu
Mafunzo hayo yameanza leo katika shule ya
Sekondari Galanosi Jijini Tanga ambayo pia yanafanyika nchi nzima
yakihusisha wasimamizi,wasimamizi wa uchaguzi na maafisa ugavi na
maafisa uchaguzi kutoka majimbo 19 ya Tanga na Kilimanjaro.
Majimbo
hayo kati yao 11 ni kutoka katika Mkoa wa Tanga na 8 ni kutoka katika
mkoa wa Kilimanjaro ambao watakwenda kusimamia uchaguzi mkuu ambao
utafanyika mwaka huu
Akizungumza wakati akifungua kikao cha
wasimamizi wa uchaguzi mkuu ,Mkurugenzi Msaidizi wa Habari na Elimu ya
Mpiga Kura NEC Dkt Cosmas Mwaisobwa kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage alisema lengo la
mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watendaji hao ili wanapokuwa
wakitekelexa majukumu yao waweze kutekelexa kwa kadri inavtyotarajiwa
kwa kuafuata taratibu zote.
Dkt Cosmas alisema kuwa pia ni
kuhakikisha hawakumbana na changamoto ambazo zinaweza kuzuia utendaji
wao kutokana na baadhi ya watendaji kuwa wapya walioteuliwa hivi
karibuni huku wakiwa hawajapata uzoefu wa kusimamia uchaguzi wowote.
“Tunalenga
kuwatumia wale ambao wana uwezo wa kusimamia uchaguzi kuwasaidia wenzao
kubadilishana uelewa wa mambo yanayohusu usimamizi wa uchaguzi “Alisema
Dkt Cosmas
Naye kwa upande wake Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa
Tanga Sebastian Masanja alisema wanawaelemisha kuhusu sheria mbalimbali
zinazoongoza uchaguzi ambazo watazitumia wakati wakisimamia uchaguzi
huo.
Masanja alisema lengo la mafunzo hayo ni kuandaa mchakato
huru na haki kwa wadau wote wa uchaguzi leo wanawafundisha sheria
mbalimbali zinazowaongoza kwa ajili uisimamiz wa uchaguzi mkuu
utakaofanyika mwezi Octoba mwaka huu.
No comments:
Post a Comment