ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 25, 2020

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZI YA MZEE MKAPA JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisaini kitabu cha maombolezi ya Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu  wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu.Benjamin William Mkapa, alipofika nyumbani kwake Mtaa wa Masaki Jijini Dar es Salaam leo 25/7/2020.kutowa mkono wa pole kwa Familia ya marehemu.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsalimia Mke wa Marehemu Mzee Mkapa. Mama Anna Mkapa, alipofika nyumbani kwa marehemu Mtaa wa Masaki kutowa mkono wa Pole kwa Familia kutokana na Kifo cha hafla cha Rais Mstaaf wa Awamu wa Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin William Mkapa, na (kushoto kwa Mama Anna)  ni Mtoto wa Marehemu Nico Mkapa.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mke wa Marehemu Mzee Mkapa Mama Anna Mkapa, alipofika nyumbani kwao mtaa wa Masiki Jijini Dar es Salaam, kutowa mkono wa pole kwa familia ya marehemu leo 25-7-2020 na kushoto kwa Mama Anna ni Mtoto wa marehemu Nico Mkapa.(Picha na Ikulu)  
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Jijini Da es Salaam, baada ya kusaini Kitabu cha maombolezi ya Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin William Mkapa, alipofika nyumbani kwa marehemu mtaa wa Masaki Jijini Dar es Salaam leo 25/7/2020, kutowa mkono wa pole kwa familia.(Picha na Ikulu)  

No comments: