ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 24, 2020

Waandishi wa habari wanawake waaswa kuzingatia sheria za uandish

Mwanahabari mkongwe, Rose Mwalimu akitoa mafunzo katika semina ya waandishi wa habari wanawake iliyoandaliwa na Tamwa. Picha na Aika Kimaro kutoka Tamwa

Asha Bani -Dar es salaam

Serikali imewataka waandishi wa habari kuzingatia taaluma yao na weledi kwa kufuata sheria ya huduma ya vyombo vya habari kuelekea katika kipindi cha uchaguzi mkuu.

Hayo yalielezwa jana Jumatano Julai 22, na mgeni rasmi ambaye ni Afisa Mwandamizi kutoka Idara Habari Maelezo, Lilian Shirima wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja ya wanahabari wanawake iliyoandaliwa na Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) kwa ufadhili wa shirika lisilo la serikali VIKES linaloendesha program ya women in newsroom.

Pia amewataka wanahabari wanawake kujiamini pindi wanapokuwa katika nafasi zao za kazi kutokana na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo.Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakisikiliza kwa makini elimu iyokuwa ikitolewa katika semina iliyoandaliwa na Tamwa

Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kushushwa thamani, kuonekana hauwezi kutekeleza majukumu yako vizuri ukilinganisha na wanaume jambo ambalo si sahihi.

Naye Mkurugenzi wa TAMWA Rose Reuben amewaeleza wanahabari hao kuwa uandishi ni safari ndefu inayohitaji uvumilivu na kujituma huku akiwataka kuangalia waliofanikiwa na kujifunza kutoka kwao kila siku.

Naye mwezeshaji katika semina hiyo mwanahabari mkongwe ambaye kwa sasa yupo GEMSAT, Rose Mwalimu alisema kuna umuhimu wa vyombo vya habari kuwepo na zingatio la usawa kwenye jinsia.

Pia aliwaambia wanahabari hao kuwa mabadiliko katika utendaji yanatakiwa kuanza na mwanahabari mwenyewe kwa kufanya juhudi mbalimbali.

No comments: