Advertisements

Tuesday, July 14, 2020

WAZIRI MHAGAMA ATOA WITO KWA VYAMA VYA SIASA KUTOWATUMIA WANAWAKE KATIKA UCHOCHEZI NA VURUGU UCHAGUZI MKUU


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Ajira Kazi Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama akizungumza na viongozi wanawake wa vyama vya siasa waliofika ofisini kwake leo jijini Dodoma Kulia kwake ni Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi.
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi akizungumza katika kikao cha Waziri Mhagama na Viongozi Wanawake wa vyama vya Siasa nchini kilichofanyika Ofisini kwake jijini Dodoma.
Kiongozi wa Viongozi Wanawake wa Vyama vya Siasa, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha UDP Bi.Saumu Rashid akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake kabla ya kukabidhi zawadi pamoja na tuzo Waziri Mhagama kwa kutambua utendaji kazi wake hafla hiyo imefanyika leo jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Umoja wa vyama 12 vya siasa ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha DP Bw.Abdul Mluya akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi zawadi pamoja na tuzo Waziri Mhagama kwa kutambua utendaji kazi wake hafla hiyo imefanyika leo jijini Dodoma.
Mwanachama wa chama cha TADEA Bi.Nuru Kimwaga,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya viongozi wenzakemara baada ya kukabidhi zawadi pamoja na tuzo Waziri Mhagama kwa kutambua utendaji kazi wake hafla hiyo imefanyika leo jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu chama cha ADC Bi.Queen Sendiga,akimpongeza Waziri Mhagama kwa niaba ya viongozi wenzake mara baada ya kukabidhi zawadi pamoja na tuzo ya kutambua utendaji kazi wake hafla hiyo imefanyika leo jijini Dodoma.
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Ajira Kazi Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama akipokea tuzo kutoka kwa Mwenyekiti wa Viongozi Wanawake wa Vyama vya Siasa, Saumu Rashid ambapo wanawake hao Viongozi walimuandalia Waziri Mhagama zawadi pamoja na tuzo ya kumpongeza kwa utendaji kazi wake.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Ajira Kazi Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (katikati) na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wanawake wa vyama vya siasa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Ajira Kazi Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (katikati) na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wanawake wa vyama vya siasa na baadhi ya wanaume waliohudhuria hafla hiyo jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Ajira Kazi Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (katikati) na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa vyama vya siasa waliohudhuria hafla ya kutunukiwa zawadi pamoja na tuzo kwa Mhe.Mhagama kwa kutambua utendaji kazi wake.

Na.Alex Sonna,Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge,Kazi,Ajira,Vijana na watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama amevitaka vyama vya siasa nchini kutowatumia wanawake Kama mawakala wa kuleta vurugu katika Uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2020.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dodoma wakati akizungumza na wanawake viongozi wa vyama hivyo katika kikao cha kumpongeza kwa namna alivyoongoza na kuimarisha vyama vya siasa kwa kuhakikisha kumekuwa umoja na mshikamano.

Aidha Waziri Mhagama amewataka viongozi wanawake wavyama vya siasa kusimamia amani na kuwa chachu ya utulivu kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Mhe.Mhagama amekutana na Viongozi wanawake kwa lengo la kumpogeza kwa kusimamia vema vyama vya siasa ambapo wizara yake ndio inayohusika na usimamizi wa vyama vya siasa kupitia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.

Waziri Mhagama amesema wanawake wana nguvu kubwa na uwezo wa kuwa viongozi na ndio maana Rais Dk John Magufuli amewaamini katika nafasi mbalimbali na hata wakati alipoteuliwa na chama chake kuwa mgombea Urais wa CCM alimchagua tena Mama Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza wake kwa mara pili.

” Nguvu yetu wanawake ni kubwa sana na kipindi hiki tunapoelekea kwenye uchaguzi nitoe rai kwenu kugombea nafasi za Uongozi kupitia vyama vyenu, chukueni fomu mkachuane kwenye majimbo na kata msiogope kwa sababu uwezo tunao”amesisitiza

Tusikubali kusubiri nafasi za upendeleo kama tuna lengo la kufikia 50/50 basi inatulazimu pia tuingie kwenye uwanja wa mapambano ili tupime nguvu zetu, na kwa sababu sisi tuna uwezo mkubwa basi naamini tutashinda,” Amesema Mhagama.

Amewataka wanawake kuwa mstari wa mbele katika kuyasema maendeleo yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano kwani yanawahusu watanzania wote bila kubagua Itikadi zao za kisiasa, kiimani na kikabila.

” Tumefikia uchumi wa kati kwa sababu pia ya utulivu wa vyama vya siasa ambavyo nyie ni viongozi, niwasihi tukahubiri pia maendeleo yetu ambayo nafahamu nyie mnayajua kwa sababu mmefanya ziara kwenye miradi inayofanywa na mmejionea kazi kubwa ambayo inafanywa,” Amesema Mhe. Mhagama.

Awali Mratibu wa wanawake viongozi wa vyama ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha UDP,Bi. Saumu Rashid amemshukuru Waziri Mhagama kwa kukubali kupokea zawadi yao na kumpongeza kwa namna ambavyo amevilea vyama vya siasa kwa muda wote wa miaka mitano.

” Tunakupongeza sana Waziri kwa ushirikiano mkubwa ambao umetupatia, hakika umekua mwema kwetu na tunakuombea urudi bungeni, sisi kama viongozi wanawake tunakuahidi tutakua mstari wa mbele kuchochea amani na utulivu kwenye uchaguzi mkuu,” Amesema Saumu.

Kwa upande wake Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amewataka viongozi hao kutoruhusu kuwa sehemu ya machafuko yanayosababishwa na baadhi ya wanasiasa wasio na uzalendo wa Nchi yao.

” Niwapongeze kwa Umoja wenu huu kama viongozi wanawake, mmekuja hapa pamoja mkiwa mmevaliwa sare moja ambayo siyo ya vyama vyenu, niwasihi Umoja huu huu ndio muende nao kwenye uchaguzi mkiweka mbele maslahi ya Nchi yetu,” Amesema Jaji Mutungi.

No comments: