Friday, December 11, 2020

MAMBO YA NJE WAMHAKIKISHIA USHIRIKIANO OLENASHA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimkaribisha Wizarani Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Ole Nasha (Mb) mara baada ya kula kiapo Ikulu tarehe 9 Desemba 2020
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi akimtambulisha Naibu Waziri Mhe. Ole Nasha kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi wakati alipowasili Wizarani
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Kabudi akimkabidhi Mhe. Ole Nasha Ilani ya Chama cha Mapinduzi kama moja ya kitendea kazi chake anapoanza majukumu yake mapya Wizarani
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi (wa tatu kushoto mstari wa kwanza) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Ole Nasha (wa nne kulia mstari wa kwanza) katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa wizara walioshiriki mapokezi ya Mhe. Ole Nasha alipowasili Wizarani baada ya kuapishwa
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Ole Nasha akisalimiana na watumishi wakati alipowasili Wizarani tayari kutekeleza majukumu yake baada ya kuapishwa. Nyuma yake ni Waziri wa Wizara hiyo Prof. Kabudi.

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wameahidi kumuonesha ushirikiano kazini Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Ole Nasha na kuhakikisha Wizara inakuwa na matokeo chanya na yenye tija kwa Taifa.

Watumishi walibainisha hayo jijini Dodoma wakati wa mapokezi ya kiongozi huyo mpya aliyeteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 05 Disemba, 2020 na kuapishwa Tarehe 09 Disemba 2020 katika viwanja vya Ikulu Jijini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) pamoja na watumishi wa Wizara walipokea Naibu Waziri, Ole Nasha alipokelewa na kumhakikishia ushikiano wa kazi ili kuiwezesha Wizara kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake. Prof. Kabudi alimhakikishia Naibu Waziri Mhe. Ole Nasha ushirikiano wake binafsi na kutoka kwa watumishi wote na kwamba uwepo wake utaongeza nguvu za kuifikisha Wizara katika viwango vya juu kiutendaji.

Itakumbukwa kuwa Disemba 05, 2020 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alifanya uteuzi wa jumla ya Mawaziri 23 pamoja na Naibu Mawaziri 23.

No comments: