ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, December 20, 2020

MHE.WAITARA AIELEKEZA NEMC KUHAKIKISHA MAENEO YA WACHIMBAJI WADOGO YANAPANDWA MITI

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mwita Waitara akizungumza na wachimbaji wadogo (hawapo pichani) alipotembelea machimbo ya Buhemba wilayani Butiama mkoani Mara. Aliyekaa kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Anna Rose Nyamubi.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mwita Waitara akikagua shughuli za uchimbaji wa dhahabu alipotembelea machimbo ya wachimbaji wadogo eneo la Buhemba wilayani Butiama mkoani Mara kwa ajili ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mwita Waitara akikagua shughuli za uchimbaji wa dhahabu alipotembelea machimbo ya wachimbaji wadogo eneo la Buhemba wilayani Butiama mkoani Mara.
Sehemu ya wachimbaji wadogo wakimisikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mwita Waitara alipofanya ziara katika eneo hilo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mwita Waitara (mbele katikati) akiwa katika ziara ya kukagua shughuli za uchimbaji wa dhahabu alipotembelea machimbo ya wachimbaji wadogo eneo la Buhemba wilayani Butiama mkoani Mara. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Butiama, Anna Rose Nyamubi.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mwita Waitara akizungumza alipowasili katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Butiama alipowasili kwa ajili ha kufanya ziara ya kutembelea machimbo ya Buhemba.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mwita Waitara ameelekeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuhakikisha maeneo ya wachimbaji wadogo yanapandwa miti.

Mhe. Waitara alitoa maelekezo hayo leo Desemba 19, 2020 wakati akizungumza na wachimbaji wadogo eneo la Buhemba wilayani Butiama Mkoa wa Mara.

Akiwa kwenye ziara hiyo ya kwa ajili ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 katika maeneo ya migodi alisema miti inakatwa Zaidi katika shughuli za uchimbaji hivyo wanapaswa kupanda kwa wingi.

Naibu waziri huyo alibainisha kuwa pamoja na jitihada za wananchi kupanda miti lakini inayopandwa inakauka kutokana na kupandwa sehemu zisizo sahihi.

Kwa mantiki hiyo alibainisha kuwa ipo haja kwa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kutoa ushauri kuhusu miti sahihi inayopaswa kupandwa badala ya kuacha wananchi kupanda miti kiholela matokeo yake inakauka.

“Tunaona mnatumia sana magogo kwa katika shughuli zenu na hiyo husababisha ukataji miti kushamiri sisi tunashauri mtumie miti inayopandwa kibiashara na si miti ya asili kwani ikipotea imepotea haitapatikana mingine,” alisisitiza.

Aidha Waitara ambaye aliambatana na watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, NEMC Kanda ya Ziwa na Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Mara alielekeza wilaya zitenge fungu kwa ajili ya zoezi la upandaji miti.

No comments: