Advertisements

Tuesday, December 1, 2020

TAKUKURU DODOMA YAREJESHA SH MILION 11 ALIZOLIPWA MAREHEMU

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Dodoma,Sosthenes Kibwengo,akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma jinsi walivyofanikisha kufakisha mahakama ya Hakimu Mkazi watu wanne pamoja na kurejesha Serikali zaidi ya sh.11 ambazo alilipwa Marehemu

Na.Alex Sonna,Dodoma

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Dodoma imefanikiwa kurejesha Serikalini zaidi ya shilingi milioni 11 ambazo zililipwa kwenye akaunti ya benki ya mtumishi marehemu kama mshahara kuanzia Oktoba 13, 2013 hadi Machi 2016 kinyume cha utaratibu.

Aidha TAKUKURU imewafikisha mahakama ya Hakimu Mkazi watu wanne na kuwafungulia mashauri mawili yenye jumla ya mashtaka 28 yanayohusu vitendo vya rushwa na kugushi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Mkuu wa Takukuru mkoani Dodoma Sosthenes Kibwengo,wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Kibwengo amesema kuwa shauri la kwanza la jinai linamkabili Aithan Chaula (61) aliyekuwa Afisa Kilimo wa halmashauri ya Chamwino na mratibu wa pembejeo za kilimo za ruzuku kwa msimu wa 2015/16 na Michael Mpembwa (44) ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Agro Suppy iliopewa uwakala wa kusambaza pembejeo za kilimo katika kijiji cha Zajilwa kilichopo wilayani humo jijini hapa.

Amesema kuwa watuhimiwa hao watashtakiwa kwa makosa 25 ya kughushi kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16.

Kibwengo amesema kuwa uchunguzi unaonyesha kuwa kati ya Januari na Agosti 2016 watuhumiwa hao waligushi nyaraka ambazo zilionyesha kwamba wakala alisambaza pembejeo zikiwemo mbegu za mahindi na mbolea kwa wakulima wa Zajilwa na hivyo kulipwa sh miloni 14 wakati wakifahamu kwamba ni uongo.

Amesema kuwa kosa hilo ni kinyume na kifungu cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007 na sheria nyinginezo.

Kibwengo ametaja shauri la pili linamkabili Benedict Mazengo (58) aliyekuwa mtendaji wa Kata ya Ntyuka na Jonathan Mwaluko (48) aliyekuwa Mwenyekiti wa mtaa wa Chimala jijini hapa ambao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya ubadhilifu kinyume na kifungu cha 28 (1) cha sheria ya kupambana na rushwa,matumizi ya nyaraka kumdanganya mwajiri kinyume na kifungu cha 22 vyote vya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007 pamoja na kugushi kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu Sura ya16.

Amesema kuwa uchunguzi wa Takukuru unaonyesha kuwa Juni 2015 watuhumiwa waligushi na kutumia nyaraka za maelezo ya uongo zilizowawezesha kutoa benki sh milion 2.9 ambazo walizitumia kwa ubadhilifu badala ya kazi iliopangwa.

Aidha Kibwengo amewasihi watumishi wa umma pamoja na wananchi kutambua kuwa rushwa ni kosa la jinai na jinai huwa haifi,hivyo wahakikishe wanakwenda kulingana na sheria,kanuni na taratibu za nchi

No comments: