Wednesday, January 6, 2021

NDOA YA KIM KARDASHAIN NA KANYE WEST YAFIKIA UKINGONI

Ndoa ya wasanii maarufu nchini Marekani Kanye West na Kim Kardashian imefika mwisho, na tayari talaka imetolewa na wawili hao wameachana rasmi.

Kwa mujibu wa Page Six wameandika Kim amechoka kuvumilia vibweka vya mumewe Kanye kitu ambacho kimemfanya adai talaka.

Mmoja wa watoa siri huyo amesema, “Wanafanya siri ila mambo yamekwisha”. hakuishia hapo aliendelea kwa kusema, “Kim ameajiri mwanasheria wa talaka Laura Wasser na wapo kwenye mazungumzo ya namna ya kumalizana.” alisema mtoa taarifa huyo.

Taarifa nyengine zilisikika zinasema Kim Kardashian na Kanye West walikuwa wakiishi kila mmoja kivyake miezi michache iliyopita.

No comments: