Watu wakiwa wamejificha ndani ya jengo la Bunge kuokoa maisha yao
Polisi wa Bunge wamethibitisha kifo cha mmoja wa afisa Polisi wao kilichotokea usiku siku ya Alhamisi kutokana na kusukumamna na wafuasi wa Rais Trump.
Ripoti inasema Afisa Brian D Sicknick amepoteza maisha kwenye kama saa 3:30 usiku wa Alhamisi kutokana na majeraha wakati alipokua kazini na uchunguzi wa kifo chake unachunguzwa na Polisi wa DC Metropolitan kitengo cha mauaji.
Afisa Sicknick amekutwa na mauti alipokua akisukumana na wafuasi wa Rais Donald Trump siku ya Jumatano January 6, 2021 na alijeruhiwa baada ya kuzidiwa nguvu na wafuasi hao na kulazimika kurudi ofisini na baadae kuzimia na kukimbizwa Hosipitali.
Mpaka sasa waliopoteza maisha katika vurugu hizo wamefikia watano, wanasiasa wengi bado wanaendelea kukemea maandamano hayo na wengi wakishininiza kujiuzulu kwa Rais Trump kwa muda huu uliobaki mpaka hapo Januari 20, 2021 kutakapokua na makabidhiano ya madaraka kwa uongozi huu na uongozi wa Rais mteule Joe Biden.
Pamoja na kwamba wengi walijua kwamba Rais Donald Trump alikua akihimiza wafuasi wakewafanye maandamano takribani wiki nzima, maafisa wa Polisi wa Bunge hawakua wamejiandaa na hili.
Wabunge hawa watunga sheria baada ya kugundua Poilisi wao wa Bunge wamezidiwa nguvu walijaribu kupiga simu majimbo ya jirani na Washington DC na moja ya simu alipigiwa Gavana wa Maryland, Larry Hogan na yeye kuwajibu tupo tayari kutuma kikosi lakini hawezi kutuma mpaka apate ruhusa kutoka kwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani.
Gavana Larry Hogan alijaribu kupiga simu kwa Waziri huyo na simu hazikujibiwa mpaka baada ya saa 1 na nusu ndipo alipopata simu kwenye namba asiyoijua ikimruhusu kupeleka Polisi kwenye jengo la Bunge.
Maryland, Virginia na Washington DC na majimbo yanayoingiliana ispokua kila jimbo lina utawala wake, kuna watu wanaishi Virginia wanafanyakazi Maryland hivyo hivyo kwenye hayo majimbo mengine watu wanafanya jimbo lingine wanaishi jimbo lingine kwa lugha nyepesi ni majimbo yanayoingiliana kwa shughuli za kila siku.
No comments:
Post a Comment