Pamoja na kwamba bado hajakubaliana kushindwa na katika uchaguzi huo, lakini amekubali kukabidhi ofisi kwa Rais mteule Joe Biden anayetarajiwa kuapishwa siku ya Alhamisi Januari 21, 2021.
Makabidhiano yanatarajiwa kufanyika Januari 20, 2021. Rais Trump pamoja na kukubali makabidhiano hayo,alikemea na kuwakana wafuasi wake walioandamana kwenye jengo la Bunge na kusema walichokifanya hakivumiliki.
Rais Trump alifahamisha kwamba pamoja na kwamba nimeshindwa katika uchaguzi wa Rais bado sikubaliani na matokeo hayo, huo ndio mwanzo wa kupiganiaa na kuifanya Amerika kuwa juu tena.
Ndani ya mjengo wa bunge bado kuna baadhi ya watunga sheria wa chama cha Republican bado nao wakipigania na kujaribu kuamini kwamba kushindwa uchaguzi wa Rais Trump kulikua na uchakachuaji kitu ambacho kinapingwa vikali na kutakiwa kuwaambia watu ukweli.
No comments:
Post a Comment