ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 31, 2021

WAZIRI BASHUNGWA AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA JWT KUJADILI NAMNA YA KUSHIRIKIANA KUKUZA SEKTA YA MICHEZO TANZAINIA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa (kulia) akizungumza wakati wa kikao baina yake na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWT Luteni Jenerali Mathew Mkingule (kushoto) wakati wa mazungumzo ya kuboresha ushirikiano kwenye sekta ya michezo baina ya jeshi na Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za Idara ya Hbari Maelezo jijini Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWT Luteni Jenerali Mathew Mkingule (kulia) baada ya mazungumzo juu ya kuboresha ushirikiano kwenye sekta ya michezo katika kikao kilichofanyika Ofisi za Idara ya Habari Maelezoi jijini Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa amekutana na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania Luteni Jenerali Mathew Mkingule na kufanya mazungumzo juu ya kuboresha ushirikiano baina ya wizara yake na Jeshi kwenye masuala mbalimbali ya michezo ikiwemo wataalamu, miundombinu ya michezo na usafiri.

Katika kikao hicho kilichofanyika Agosti 31, 2021 jijini Dodoma, Waziri Bashungwa amemweleza Mnadhimu huyo nia ya Wizara ya Habari kushilikiana na jeshi hilo katika kuinua sekta ya michezo kwa kuwashirikisha wataalamu mbalimbali wa michezo ambao wapo katika majeshi mbalimbali hapa nchini ili waweze kuibua na kuendeleza vipaji vya wanamichezo.

Waziri Bashungwa amesema Wizara yake imeona ni vyema kuwa na michezo ya kikamkati (Kipaumbele) ili kujikita zaidi kwenye michezo hiyo na kuweza kushindana kimataifa, akisema kufanya hivyo kutairudisha Tanzania katika historia ya baadhi ya watanzania waliowahi kufanya vyema katika baadhi ya michezo kimatafifa.

“Tunaamini kwa kushirikiana na jeshi, timu za Taifa zitaweza kufanya kambi katika maeneo ya jeshi, hii itaongeza nidhamu na ukakamavu wa timu zetu” Amesem Waziri Bashungwa.

Kwa upande wake Luteni Jenerali Mathew Mkingule amesema mazungumzo hayo ni hatua nzuri katika kukuza sekta ya michezo akisema anaipeleka taarifa ya mazungumzo hayo kwa Mkuu wa Majeshi kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

Aidha, viongozi hao kwa pamoja wamekubaliana Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kukutana na uongozi wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) ili kujadiliana namna bora na sehemu za kipaumbele za kushirikiana.

Mwisho.

WAZIRI MKUU AZINDUA TAWI LA BENKI YA MWANGA NA KUTOA MAAGIZO SABA

 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Tawi la Benki ya Mwanga Hakiki jijini Dodoma, Agosti 31, 2021.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt Benard Kibessa (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Benki ya Mwanga Hakika, Ridhiwani Mringo tawi la Dodoma, baada ya kuzindua tawi hilo Agosti 31, 2021.Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi pamoja na watumishi wa Benki ya Mwanga Hakika baada ya kuzindua tawi la Benki hiyo jijini Dodoma, Agosti 31, 2021. Waliokaa kutoka kushoto ni Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda, Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Ridhiwani Mringo, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Benard Kibessa na kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO AVITAKA VYUO KUTOA ELIMU INAYOENDANA NA SOKO LA AJIRA

Naibu waziri wa fedha na mipango ,Hamad Masauni wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa chuo Cha uhasibu Arusha( IAA) wakati alipotembelea chuo hicho kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa chuoni hapo (Happy Lazaro)
Aliyeko kushoto ni Mkuu wa chuo Cha uhasibu Arusha,Profesa Eliamani Sedoyeka akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa fedha na mipango Hamad Masauni wakati alipotembelea chuo hicho kujionea miradi mbalimbali inayoendelea chuoni hapo (Happy Lazaro)

Happy Lazaro,Arusha.

Arusha.NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Hamad Yussuf Masauni, amevitaka vyuo nchini kutoa elimu inayoendana na uhitaji wa soko la ajira kwa kuwaandaa vijana kuweza kujiendeleza wenyewe .

Ameyasema hayo wakati alipotembelea chuo cha uhasibu Arusha (IAA) na kukagua majengo matatu yatakayokuwa na maktaba ya vitabu, mabweni na sehemu ya chakula.

Masauni amesema kuwa ,ni vizuri vyuo vikajikita katika kutoa elimu ambayo itawezesha kuwaandaa vijana kukabiliana na changamoto ya ajira huku wakiwaondolea dhana ya kusubiri kuajiriwa badala yake wajiandae kujiajiri.

DKT. CHAULA AZUNGUMZIA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA MTOTO WA KIKE

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula (katikati) akizindua tovuti ya shirika lisilo la Serikali la Action Girls Foundation, jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika hilo Rabia Saad na wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Afya na Lishe wa TAMISEMI Dkt. Ntuli Kapologwe
atibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula (katikati), Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama Mtandao wa Wizara hiyo Eng. Steven Wangwe (kushoto mstari wa nyuma) Mkurugenzi wa Shirika hilo Rabia Saad (kushoto mstari wa mbele), Mkurugenzi wa Huduma za Afya na Lishe wa TAMISEMI, Dkt. Ntuli Kapologwe (wa pili kulia) na wakifurahia baada ya uzinduzi wa tovuti ya shirika lisilo la Serikali la Action Girls Foundation, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula (katikati) akizungumza kabla ya kuzindua tovuti ya shirika lisilo la Serikali la Action Girls Foundation, jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika hilo Rabia Saad akifuatiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama Mtandao wa Wizara hiyo Eng. Steven Wangwe na wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Afya na Lishe wa TAMISEMI Dkt. Ntuli Kapologwe

MATUKIO KATIKA PICHA WAKATI WA BUNGE LEO AGOSTI 31,2021 JIJINI DODOMA

Spika wa Bunge, Job Ndugai akiingia Bungeni kuongoza Bunge la 12 Mkutano wa Nne Kikao cha Kwanza Jijini Dodoma
Spika wa Bunge, Job Ndugai akiongoza Bunge la 12 Mkutano wa Nne Kikao cha Kwanza Bungeni
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Selemani Jafo (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Uwekezaji, Mhe. Geoffrey Mwambe wakati wa Bunge la 12 Mkutano wa Nne Kikao cha Kwanza Bungeni Jijini Dodoma,
Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Mhe. Emmanuel Mwakasaka akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo wakati wa Bunge la 12 Mkutano wa Nne Kikao cha Kwanza Jijini Dodoma,
Waheshimiwa Wabunge wakisimama kumkumbuka aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hayati Elias Kwandikwa wakati wa kikao cha kwanza cha Mkutano wa Nne wa Bunge la 12 Bungeni Jijini Dodoma
Waheshimiwa Wabunge wakishiriki kikao cha kwanza cha Mkutano wa Nne wa Bunge la 12 Bungeni Jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deo Ndejembi akijibu hoja za Waheshimiwa Wabunge wakati wa Bunge la 12 Mkutano wa Nne Kikao cha Kwanza Bungeni Jijini Dodoma,
Wanakwaya wa ofisi ya Bunge wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa ufunguzi wa Bunge la 12 Mkutano wa Nne Kikao cha Kwanza Bungeni Jijini Dodoma, Agosti 31, 2021

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

MHE. RAIS SAMIA AANZA RASMI KUREKODI KIPINDI KITAKACHOTANGAZA UTALII, BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akijumuika pamoja na Wananchi mbalimbali Nchini katika Ukumbi wa Mji Mkongwe Zanzibar leo Agosti 29,2021, alipokua akianza rasmi kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akijumuika pamoja na Wananchi mbalimbali Nchini katika Ukumbi wa Mji Mkongwe Zanzibar leo Agosti 29,2021, alipokua akianza rasmi kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Msanii Mkongwe wa Taarab Asilia Nchini Bibi Mariam Hamdani, alipokutana nae katika Ukumbi wa Mji Mkongwe Zanzibar leo Agosti 29,2021, kabla ya kuanza rasmi kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Utalii na mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Mussa, wakati wa kuanza kurekodi rasmi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini katika Ukumbi wa Mji Mkongwe Zanzibar leo Agosti 29,202. PICHA NA IKULU.

Siku ya Mwananchi, Waziri Bashungwa aipongeza Yanga na Mashabiki wake


 

UYOGA WA TANZANIA KUPATA SOKO NCHINI UHOLANZI

Balozi Irene Kasyanju (katikati) akiwa katika mazungumzo na uongozi wa LIMAX Group ulioongozwa na Mkurugenzi na Mmiliki wa Kampuni hiyo, Bw. Tom van WALSEM (wa pili kushoto) kuhusu soko la uyoga wa Tanzania nchini Uholanzi kwenye Ofisi za Kampuni hiyo zilizopo katika Mji wa Horst, Uholanzi. LIMAX Group inazalisha faida/pato kwa mwaka (annual turnover) la takriban Euro milioni 25.
Balozi Irene Kasyanju (kulia) akiangalia namna uyoga unavyofungashwa kwenye
makasha (packaging) tayari kwa kupelekwa sokoni huku akipatiwa maelezo ya mchakato
mzima wa ufungaji kutoka kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa LIMAX Group, Bw. Rob
Menheere (kushoto). Katikati ni Bw. Petro Mahuwi “intern” Mtanzania aliyeongozana
na Balozi Kasyanju kwenye ziara hiyo.
Namna kitalu kimoja wapo cha uyoga uliopandwa na ambao
unakaribia kuvunwa kinavyoonekana katika moja ya mashamba makubwa 4 ya LIMAX
Group iliyoko Horst, Uholanzi.
Balozi Kasyanju (kushoto) akiwa na Mkurugenzi na Mmiliki wa LIMAX Group,
Bw. Tom van WALSEM (wa kwanza kushoto); Mkurugenzi Mwendeshaji, Bw. Rob
Menheere (wa pili kushoto); na Meneja Biashara, Bw. Mark Duppen (wa tatu
kushoto) wakikamilisha mazungumzo yao baada ya zoezi la kutembelea mashamba ya uyoga
mjini Horst, Uholanzi kukamilika.

UYOGA WA TANZANIA KUPATA SOKO NCHINI UHOLANZI

Kampuni maarufu
ya Uholanzi, LIMAX B.V. (LimaxGroup) imedhamiria kuwekeza kwenye Sekta ya Uyoga
nchini Tanzania kwa kujenga kiwanda cha kusindika na kukausha uyoga Mkoani
Iringa kwa thamani ya Euro milioni 2.1 ambazo ni sawa na Shilingi Bilioni 5.5
za Tanzania. Hayo yameelezwa kufuatia Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe.
Irene Kasyanju kutembelea kampuni hiyo tarehe 26 Agosti 2021 na kufanya
mazungumzo na Mkurugenzi na Mmiliki wa kampuni hiyo, Bw. Tom VanWalsem.

WALIOJIMILIKISHA ARDHI KIHOLELA SIMANJIRO WAONDOLEWA UMILIKI

Na Mwandishi wetu, Simanjiro

Wananchi 27 waliojimilikisha bila uhalali ekari 12,000 ya maeneo ya ardhi ya Kijiji cha Emboreet Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wamenyang’anywa ardhi hiyo na kurejeshwa mikononi mwa Serikali ya Kijiji hicho.

Wananchi hao 27 walijimilisha ekari 1,000 na wengine ekari 500 tangu mwaka 1993 bila kuwa na nyaraka zozote zinazowaruhusu kumiliki.

Kamishina msaidizi wa ardhi wa mkoa wa Manyara, Leonard Msafiri ametoa uamuzi huo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Emboreet.

Msafiri amesema endapo wananchi hao bado wanahitaji ardhi hiyo wawasilishe maombi na yajadiliwe upya na taratibu zifuatwe.

Amesema eneo hilo lilitengwa katika mpango wa matumizi ya ardhi ya Emboreet ambapo matumizi hayakinzani na masuala ya hifadhi ya wanyama pori.

WAZIRI JAFO ATOA MIEZI SITA KWA MAKAMPUNI YA MOTISON GROUP KUTENGA ENEO LA KUHIFADHIA BIDHAA ZA VINYWAJI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani jafo akikagua mfereji wa maji yaliyotibiwa kwenye kampuni ya vinywaji baridi ya Coca Cola kwanza Jijini Dar Es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani jafo akitoa maelekezo kwa viongozi wa kiwanda cha Iron & Steel kuhusu kufunga mtambo maalumu wa kuzuia moshi kuzagaa kwenye mazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo ametoa miezi sita kwa wamiliki wa kiwanda Cha Sayona kinachomilikiwa na Kampuni ya Motison Group ambacho kinazalisha bidhaa za plastiki, rangi na Chuma kuhakikisha kinatenga eneo maalumu la kuhifadhia bidhaa za vinywaji ili kuepuka kuchanganyika na bidhaa zisizo za chakula zinazo zalishwa kiwandani hapo.

Ameyasema hayo alipofanya ziara kwenye kampuni ya Motison Group inayomilikiwa na kampuni ya Sayona, Mikocheni Jijini Dar es Salaam.

Monday, August 30, 2021

EAC SECRETARY GENERAL URGES PARTNER STATES’ GOVERNMENTS TO INVEST IN INDUSTRIAL PARKS



 

East African Community Headquarters, Arusha, Tanzania, 30th August, 2021: The East African Community (EAC) Secretary General, Hon. Dr. Peter Mathuki, is urging EAC Partner States’ governments to invest in industrial parks and infrastructure to improve the competitiveness of the region and increase Intra-EAC trade.

 

Speaking during the opening session of the East Africa Trade and Industrialization Week (EATIW 2021), held at the Julius Nyerere Convention Centre, in Dar es Salaam, Tanzania, Dr. Mathuki urged EAC Partner States’ governments to enhance industrial productivity and strengthen institutional frameworks and policies to accelerate economic growth in the region.

 

“Currently, manufacturing contributes to GDP a meagre 8.9%. To achieve the set target of 25% in 2032, there is a need for diversification of the manufacturing base and raising local value-added content resource-based exports,” he said.

 

The Secretary General called for promotion of rural industrialization through an agricultural development led industrialization strategy and strengthening of research, technology and innovation capabilities of all EAC Partner States, to foster structural transformation of the manufacturing sector and industrial upgrading. 

 

As a strategy towards economic recovery amid Covid-19 in the region, Dr. Mathuki called upon EAC Partner States Governments to offer long-term stimulus packages for private sector development and sector-specific incentives for the established regional value chains such as cotton, textile and apparel, leather livestock and Agro-processing. 

 

“Instead of competing, EAC Partner States need to complement each other. Harnessing our comparative advantage by collectively improving infrastructure connectivity will fast-track regional development,” Dr. Mathuki added. 

 

The Secretary General also reaffirmed EAC´s commitment to finalize the Common External Tariff (CET) before the end of 2021. 

 

“The EAC is committed to finalising the Common External Tariff (CET) by the end of the year, in a move set to promote the Community´s domestic industries & safeguard the region from international shocks,” he said. 

 

The 38th Meeting of the Sectoral Council of Ministers on Trade, Industry, Finance and Investment (SCTIFI), which was held on 26th May 2021, adopted a four-band CET structure (0%, 10% and 25%).  

 

The Secretary General said emphasised the need for EAC Partner States Governments to speed up the finalisation and implementation of EAC Regulations on liberalisation of air transport services, in a move set to lower flight costs and in turn reduce the cost of doing business in the region. 

 

“With only about 2% of East Africans vaccinated, it is critical that the private sector leads deliberate public campaigns on Covid-19 vaccination and jointly to enhance EAC as an investment destination,” Dr. Mathuki said.  

 
 

On his part, Mr. David Osiany, Chief Administrative Secretary, Ministry of Industrialization, Trade and Enterprise Development, Republic of Kenya, called for consistent public-private sector dialogues and collaboration to develop policies corresponding with the current business environment. 

 

In his remarks, Hon. Prof. Kitila Mkumbo, Minister for Industry and Trade, United Republic of Kenya called for joint investment by EAC Governments and the Private sector in skills development. 

 

“Only 50% of our workforce are employable in the current job market. The public-private sector should come up with a strategy on skills development to fill this gap,” said Prof. Mkumbo. 

 

The East African Trade & industrialization week which officially commenced today will run up to the 3rd of September, 2021. The conference brings together business operators, policy makers, civil society leaders, international and UN organization leaders, academia from all avenues to address challenges and propose solutions to the changing role of business in the region and the continent.  

NAIBU WAZIRI GEKUL AZINDUA RASMI KAMATI YA TAMASHA LA MICHEZO LA WANAWAKE

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (aliyekaa katikati) akizungumza na wajumbe wa kamati ya maandalizi ya Tamasha la Michezo la Wanawake pamoja na waandishi wa Habari mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (kakatikati) akizungumza na wajumbe wa kamati ya maandalizi ya Tamasha la Michezo la Wanawake pamoja na waandishi wa Habari (hawapo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam Wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Tamasha la Michezo la Wanawake, Neema Msitha (kulia) ambaye ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (katikati) wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo toka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yusuph Singo.

SPIKA NDUGAI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI JIJINI DODOMA

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiongoza kikao cha kamati ya uongozi kilichopokea na kupitisha hati ya dharura na kujadili Shughuli za Mkutano wa Nne wa Bunge pamoja na mapendekezo ya ratiba ya Mkutano kikao kilichofanyika leo katika Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma,
Naibu Spika, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya uongozi kilichopokea na kupitisha hati ya dharura na kujadili Shughuli za Mkutano wa Nne wa Bunge pamoja na mapendekezo ya ratiba ya Mkutano kikao kilichofanyika leo katika Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akichangia jambo wakati kikao cha kamati ya uongozi kilichopokea na kupitisha hati ya dharura na kujadili Shughuli za Mkutano wa Nne wa Bunge pamoja na mapendekezo ya ratiba ya Mkutano kikao kilichofanyika leo katika Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma, Agosti 30, 2021, kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof. Aderladus Kilangi
Wajumbe wa kamati ya uongozi wakiwa katika kikao cha kamati hiyo kilichopokea na kupitisha hati ya dharura na kujadili Shughuli za Mkutano wa Nne wa Bunge pamoja na mapendekezo ya ratiba ya Mkutano katika kikao kilichofanyika leo katika Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma, Agosti 30, 2021

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

SERIKALI YA BURUNDI YAPEWA ENEO LA KUJENGA BANDARI KAVU

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ( Sekta ya Uchukuzi) Bw. Gabriel Migire akisaini makubaliano ya awali ya kuipatia Nchi ya Burundi eneo la Kujenga Bandari kavu, Kwala, mkoani Pwani.
Katibu Mkuu wizara ya Ujenzi na Uchukuzi( Sekta ya Uchukuzi) Bwa.Gabriel Migire (kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Biashara,Uchukuzi, Viwanda na Utalii wa Burundi Bw. Jeremie Banigwaninzigo, wakionyesha hati ya makubaliano ya awali ya kupeana eneo la kujenga Bandari kavu, Kwala, mkoani Pwani, kwa ajili ya nchi ya Burundi.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe kutoka nchi za Tanzania na Burundi, mara baaada ya kufanya kikao cha maandalizi ya Tanzania kuipatia Burundi eneo la kujenga Bandari Kavu eneo la Kwala, mkoani Pwani.

Picha na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

Serikali ya Burundi imeishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuipatia enao la hekta kumi kwa ajili ya kujenga Bandari kavu eneo la Kwala, mkoani Pwani.

Hayo yamesemwa na Balozi wa Burundi nchini Tanzania Bw. Gervais Abayeho, wakati wa kikao cha pamoja kilichowakutanisha Balozi huyo pamoja na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mtumba, jijini Dodoma.

MKUTANO WA NJIA YA MTANDAO WA WAZIRI MULAMULA NA WANADIASPORA, WASHINGTON, DC

WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI BALOZI LIBERATA MULAMULA AKIFANYA ZIARA YA KIKAZI NCHINI MAREKANI  AUG 25-29
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia maswala ya Afrika, Mhe. Victoria Nuland (nguo ya mabaka nyeusi na yeupe) pamoja na kaimu Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulika na maswala ya Afrika, Balozi Robert Godec (wapili toka kulia). Katika mazungumuzo hayo, viongozi hao walijadili maswala mbalimbali ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Marekani likiwemo janga la Uviko-19, biashara na uwekezaji.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia maswala ya Afrika, Mhe. Victoria Nuland (nguo ya mabaka nyeusi na yeupe) pamoja na kaimu Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulika na maswala ya Afrika, Balozi Robert Godec (wapili toka kulia). Katika mazungumuzo hayo, viongozi hao walijadili maswala mbalimbali ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Marekani likiwemo janga la Uviko-19, biashara na uwekezaji.
Wliokaa kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Mb) akiwa na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani Bi. Jean Msabila pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya Balozi Swahiba Mndeme na Mabalozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Marekani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na Mkurugenzi idara ya Amerika na Ulaya Balozi Swahiba Mdeme ( wakwanza kushoto), Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani Bi. Jean Msabila (watatu toka kushoto) katikapicha ya pamoja na Bw. Robert A. Raines, Naibu Balozi wa Marekani nchini Tanzania. kulia ni Dkt. Elias Magembe.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

MAJALIWA AZINDUA OFISI ZA FFU MKOA WA SINGIDA NA MAKAO MAKUU YA POLISI MKOA WA SINGIDA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua majengo ya Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Singida na Ofisi ya Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Singida, ambayo yamegharimu shilingi1.314 ,
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipofungua jengo la Ofisi ya Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Mkoa wa Singida Agosti 30, 2021. Kutoka kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Stella Mutabihirwa, Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro na Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kufungua jengo la Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Singida Agosti 30, 2021. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Stella Mutabihirwa, kulia ni Mkuu wa Moa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na wa pili kulia ni Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro