Aliyekua msemaji wa Club ya wekundu Msimbazi, Simba Sports Club leo katika mkutano wa Yanga na waandishi wa habari ametangaza rasmi kujiunga na Yanga timu pinzani na Simba na wakati akiwa msemaji wa Simba alikua akiikandia sana timu hiyo.
Katika mkutano huo wa waandishi wa habari uliofanyika katika hotel ya Serena ya jijini Dar es Salaam, Haji Manara baada ya kutambulishwa, na Senzo Masingiza, alijitangaza rasmi kwamba yeye sasa ni msemaji wa Yanga.
Mkutano huo ambao ulijaa sana na waandishi wa habari wengi hawakutegea kitu kama hicho kingetokea, lakini ndio maisha ya mpira na ifikie wakati maisha ya wa semaji wa club waifanye iwe kazi na sio ushabiki wa timu.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake