Jeshi la Polisi mkoa wa Dar es Salaam limefanikiwa kumdhibiti Mtu mmoja ambaye alikua anafyatua ovyo risasi hewani karibu na Ubalozi ws Ufaransa,
Kamanda wa Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema Askari wawili wa jeshi la polisi nchini ambao walikuwa doria katika eneo hilo wamepigwa risasi na mtu asiyejulikana mwenye asili ya kisomali na kusababisha vifo vya askari hao lakini pia raia huyo amefariki baada ya yeye pia kushambuliwa na risasi.
Amesema watafuatilia kujua uraia wa mtu huo na baadae kutoa taaria zaidi
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake