ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 17, 2021

WAZIRI MRAMBA AFARIKI DUNIA

ALIYEWAHI kuwa Waziri wa Fedha wa Tanzania na Mbunge wa Rombo, Basil Pesambili Mramba amefariki dunia leo Jumanne, Agosti 17, 2021 katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu.

Mramba ambaye alizaliwa Mei 15, 1940 aliwahi kuwa Waziri wa Fedha katika utawala wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambapo aliiongoza Wizara hiyo mwaka 2001-2005, baadaye Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko mwaka 2006 hadi 2008.

Mtoto wa Mramba, Godfrey Mramba amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kueleza kuwa ni wanafamilia wachache wataruhusiwa kufika kutoa pole nyumbani kwa marehemu, Mawenzi Road, Oysterbay jijini Dar.

Taarifa ya familia

Born: 15th May, 1940. Departed: 17th August, 2021.
Kwa masikitiko makubwa, Familia ya Mramba inatangaza kuondokewa na baba yao mpendwa, Basil Pesambili Mramba; maisha yake yamekuwa mazuri hapa duniani na atakumbukwa kwa mazuri.

Mzee alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Regency Medical Center, mapema hii leo Agosti 17, 2021 ametutoka.

Kutokana na janga kubwa lililopo, familia inapokea salam zenu za pole pamoja na sala zenu, tunaomba faragha kutokana na msiba huu. Tutapokea ndugu wa familia PEKEE katika nyumbani kwake, Mawenzi Road, Oysterbay. Taarifa zaidi kuhusu msiba huu zitatolewa baadaye.

Bwana alitoa, Bwana Ametwaa, Jina lake lihimidiwe. Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani. Amen.

Godfrey B. Mramba.wa GPL

No comments: