Tuesday, August 17, 2021

YANGA YAANZA KUJIFUA MOROCCO TAYARI KWA MSIMU UJAO

Kipa mpya wa Yanga Djigui Diara kutoka Mali akipasha leo kwa mara ya kwanza tangu usajili wake Yanga akiwa Morocco na timu yake mpya ya Yanga. Timu ya Yanga iliwasili jana nchini humo kujiandaa na msimu ujao wa ligi ikiwemo ligi ya mabingwa Africa,
Mcheazji Saido Ntibazonkiza akiwa nae katika viwanja vya mazoezi nchini Morocco katika kambi ya Yanga.
Mchezaji Djuma Shaban nae akipasha misuli kwa mara ya kwanza akiwa na klabu ya Yanga nchini Morocco
Mchezaji Fiston Mayele usajili mpya Yanga akipasha na timu yake hiyo mpya katika uwanja wa mazoezi nchini Morocco
Mchezaji kinda Yusuph Athumani aliyesajiliwa na Yanga kutokea Biashara United ya Mara akijumuika na wachezaji wenzake wa  Yanga nchini Morocco
Kipa Erick Johora usajili mwingine mpya Yanga akipiga jalamba katika uwanja wa mazoezi Morocco
Yacouba Songne akiwa tayari Morocco alipojiunga na timu yake akitokea Burkina Faso nchini kwake alipokua ameenda kwa mapumziko ya wiki mbili,
Beki Adeyun Saleh beki wa kushoto wa Yanga akijiunga katika uwanja wa mazoezi wa Yanga nchini Morocco,
Mchezaji wa Yanga kiungo matata sana Feisal Salum (Fei Totot) akiwa katika uwanja wa mazoezi wa Yanga nchini Morocco, Yanga iptakua Morocco kwa siku 10 wakijiandaa na msimu wa 2021/2022 na timu inatarajiwa kurejea nchini Aug 27, 2021 tayari kwa siku ya Mwananchi itajayofanyika siku ya Jumapili Aug 29, 2021 katika uwanja wa Mkapa,

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake