Tuesday, April 19, 2022

FILAMU YA ROYAL TOUR YAZINDULIWA NEW YORK


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kabla ya uzinduzi wa filamu ya Tanzania The Royal Tour katika ukumbi wa Guggenheim Museum, New York nchini Marekani leo tarehe 18 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mwandaaji wa filamu ya Royal Tour na Baadhi ya Wafanya Biashara wa Nchini Marekani baada ya Futari Jijini New York Marekani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mtangazaji Maarufu wa Kituo cha Television cha CBS nchini Marekani Bi. Gayle King wakati alipokutana na Wafanyabiashara, Wawekezaji pamoja na Wadau Wakuu wa Sekta ya Habari wa nchini Marekani katika Jiji la New York leo tarehe 18 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akitazama Filamu ya Royal Tour pamoja na Wageni mbalimbali mashuhuri New York nchini Marekani leo tarehe 18 Aprili, 2022.
Kikundi cha Ngoma za asili kutoka Bagamoyo kikitumbuiza katika uzinduzi wa filamu ya Tanzania The Royal Tour katika ukumbi wa Guggenheim Museum, New York nchini Marekani leo tarehe 18 Aprili, 2022.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake