Na Timothy Itembe Mara.
Serikali kupitia vyombo vyake imeombwa kutatua kero mbalimbali zinazokabili magereza ikiwemo kupunguza mlundikano wa mahabusu na wafungwa na ucheleweshwaji wa kesi.
Mbunge wa jimbo la Tarime,Michael Kembaki alisema hayo wakati akikabidhi misaada mbalimbali katika Gereza la wilaya Tarime mkoani Mara siku moja baada ya Rais wa Jamuhuri ya muungano ya Tarnzania,Samia Suluhu Hassani kutoa msamaha kwa wafungwa 3826 Tanzania.
Kwa Taarifa ilyotolewa kwa vyombo vya habari na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni kuwa msamaha huo unaenda sambamba na masharti mbalimbali ikiwa ni pamoja na wafungwa wote kupunguziwa robo ya vifungo vyao baada ya punguzo la kawaida la moja ya tatu linalotolewa chini ya kifungu cha 48(1) cha Sheria ya Magereza.
Katika hafla hiyo Kembaki alikabidhi misaada ya TV Ichi 50 yenye dhasmani ya shilingi Milioni 1.3,mifuko ya saruji 50 yenye dhamani ya shilingi milioni 1.1,katoni 40 za soda zenye dhamani ya shilingi 400,000 na katoni 40 za miche ya sabuni wakati huo huo aliomba kupewa thamani ya fedha ya tofali za ujenzi wa kituo cha Afya cha Gereza kinachojengwa ili kugarimia.
Kembaki alisema kuna haja serikali kutazama upya swala la mlundikano wa mahabusu na wafungwa ndani ya Gereza la Tarime na kulitafutia ufumbuzi pia aliomba vyombo vya serikali vinavyohusika kumsaidia mmoja wa mahabusu ndani ya gereza hilo ambaye anakabiliwa na kesi ya mauaji ikiwemo wizi wa kutumia nguvu ambaye amekaa zaidi ya miaka 11 bila kesi yake kutolewa uwamuzi.
Kwa upande wake mkuu wa Gereza la wilaya Tarime ASP Sebastian Dioniz alibainisha kesi inayomkabili mahabusu huyo ambaye jina limehifadhiwa,kuwa ni Mauaji pamoja na kesi ya wizi wa kutumia nguvu (Roberi) ambapo amekaa Gerezani hapo kwa muda mrefu bila ya kesi yake kutolewa hukumu.
Diwani vitimaalumu katika halmashauri ya mji wa Tarime Doris Chacha alisema kuna haja serikali kuangalia umuhimu wa haki za wafungwa na mahabusu ili kuondokana na kero mbalimbali ambazo hazina sababu zinazolikumba gereza hilo.
Imebainika kuwa ndani ya gereza hilo kuna jumla ya wagungwa 153 na mahabusu 292 ambapo jumla lina wahalifu 445 huku gereza hilo likiwa na uwezo wa kuhifadhi wahalifu 209 na kuwa idadi hiyo inasababisha kuwepo na mlundikano ndani ya Gereza.
.jpg)
.jpg)
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake