Thursday, April 28, 2022

ROYAL TOUR NI LANGO KUU LA FURSA KATIKA UTALII- BALOZI DKT. PINDI CHANA


Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Mhe Balozi Dkt Pindi Chana, ametoa wito kwa watanzania kukaa tayari kwa kuchangamkia furusa mbalimbali zitakazo tokana na matokeo chanya ya Filamu ya Royal Tour inayo tarajiwa kuzinduliwa Jijini Arusha.

Mhe Chana ameyasema hayo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, alipo wasili tayari kuudhuria uzinduzi wa Filamu hiyo muhimu kwa sekta ya Utalii nchini.
“Royal Tour Arusha inakwenda kufungua zaidi furusa za Utalii nchini, Mhe Rais wetu Mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan ametufungulia furusa hii, sasa sote tukae katika mkao wa kunufaika nayo” Mhe Chana
Na katika hatua nyingine Mhe Chana amekagua ukumbi wa utakaotumika kuzindulia Filamu hiyo na kuridhishwa na maandalizi hayo.
‘Filamu ya Royal Tour inatarajiwa kuzinduliwa Jijini Arusha hapo kesho.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake