ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 31, 2024

AFRIKA TUMIENI VEMA FURSA ZA SOKO LA AFCFTA


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) (kulia) Januari 30, 2024 akifungua Mkutano wa 13 wa Mawaziri wa Biashara AfCFTA unaofanyika Durban, Afrika Kusini, kuanzia tarehe 30 hadi 31 Januari 2024 ambapo Tanzania, ni Mwenyekiti wa Mikutano ya AfCFTA kwa mwaka huu 2024.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) (kulia) akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa AfCFTA Mhe. Wamkele Mene baada ya kufungua Mkutano wa 13 wa Mawaziri wa Biashara AfCFTA unaofanyika Durban, Afrika Kusini, kuanzia tarehe 30 hadi 31 Januari 2024 ambapo Tanzania, ni Mwenyekiti wa Mikutano ya AfCFTA kwa mwaka huu 2024.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) na Mwenyekiti wa Mkutano wa 13 wa Mawaziri wa Biashara wa Eneo Huru la Biashara Afika (AfCFTA) amezisitiza Nchi Wanachama wa Mkataba huo kutumia vema fursa zilizopo ili kukuza biashara.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo Januari 30, 2024 alipokuwa akifungua Mkutano wa 13 wa Mawaziri wa Biashara AfCFTA unaofanyika Durban, Afrika Kusini, Mkutano huo ambao utafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 30 hadi 31 Januari 2024.

TANZANIA YAPOKEA MSAADA WA Sh. TRIL 1.4 KUTOKA GLOBAL FUND




Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameki Nchemba Madelu (Mb), (kushoto) na Mkuu wa Global Fund- Afrika, Bw. Linden Morrison, wakisaini Hati za Mikataba ya Msaada yenye thamani ya takribani dola za Marekani milioni 606.9 (saa na zaidi ya shilingi trilioni 1.4) kwa ajili ya kupambana na maradhi ya UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na Uimarishaji wa mifumo ya afya nchini, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Kambarage, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameki Nchemba Madelu (Mb), (kushoto) na Mkuu wa Global Fund- Afrika, Bw. Linden Morrison wakibadilishana Hati za Mikataba ya Msaada yenye thamani ya takribani dola za Marekani milioni 606.9 (zaidi ya shilingi trilioni 1.4) kwa ajili ya kupambana na maradhi ya UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na Uimarishaji wa mifumo ya afya nchini, hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kambarage, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameki Nchemba Madelu (Mb), (kushoto) na Mkuu wa Global Fund- Afrika, Bw. Linden Morrison, wakionesha Hati za Mikataba ya Msaada yenye thamani ya takribani dola za Marekani milioni 606.9 kwa ajili ya kupambana na maradhi ya UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na Uimarishaji wa mifumo ya afya nchini, hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kambarage, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameki Nchemba Madelu (Mb), akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini Hati za Mikataba minne ya Msaada yenye thamani ya takribani dola za Marekani milioni 606.9 (sawa na zaidi ya shilingi trilioni 1.4) kutoka Mfuko wa Dunia (Global Fund) kwa ajili ya kupambana na maradhi ya UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na Uimarishaji wa mifumo ya afya nchini, hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kambarage, jijini Dodoma.

WAZIRI MAKAMBA ANADI FURSA ZA BIASHARA, UWEKEZAJI ITALIA



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amenadi fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana nchini katika mkutano wa wafanyabiashara, viongozi wa siasa na wa kijamii nchini Italia.

Katika mkutano huo, Waziri Makamba amewaeleza wafanyabiashara na wawekezaji wa Italia fursa mbalimbali za biashara zinazopatikana nchini pamoja na mageuzi makubwa ya kuboresha mazingira ya uwekezaji yanayofanyika chini ya Uongozi imara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Waziri Makamba amesema mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ni salama na rafiki kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ili kuhakikisha wafanyabiashara wanatekeleza majukumu yao katika mazingira rafiki na salama.

Kadhalika Waziri Makamba amesema kuwa Tanzania inazingatia misingi ya utawala bora pamoja na kuzungukwa na nchi saba ambazo hazina bandari na hivyo kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na huduma kwenda katika nchi hizo.

SERIKALI YAANZA KUFANYA TATHIMINI KUBAINI MAENEO YATAKAYOBORESHWA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MAZINGIRA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akijadiliana jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni katika Kikao cha pili Mkutano wa 14 wa Bunge Jijini Dodoma leo Januari 31, 2024.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akijibu maswali bungeni jijini Dodoma leo Januari 31, 2024 kuhusu mkakati wa Serikali wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi, katika Kikao cha pili Mkutano wa 14 wa Bunge.

Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wizara za kisekta imeanza kufanya tathmini nchi nzima kubainisha maeneo yanayohitaji kufanyiwa maboresho kukabiliana na athari za kimazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtambwe Mhe. Khalifa Mohammed Issa aliyetaka kujua lini Serikali itafanya utafiti kuyabaini maeneo yaliyoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.

SERIKALI YAWALIPA WAZABUNI TRIL 2.1 KWA MWAKA 2016 HADI 2023


Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akijibu swali la Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina, kuhusu kiasi cha fedha ambacho Serikali imewalipa 2023 wazabuni na wakandarasi wa ndani baada ya kuwasilisha madai yao na kufanyiwa uhakiki, bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (kulia), bungeni Jijini Dodoma.

Na. Khadija Ibrahim, WF, Dodoma
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ameliambia Bunge, Mjini Dodoma kuwa katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2016/2017 hadi Desemba 2023, imewalipa wazabuni na wakandarasi wa ndani zaidi ya shilingi trilioni 2.1 kati ya madai ya zaidi ya shilingi trilioni 3.1 yaliyowasilishwa.

Dkt. Nchemba amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina, aliyetaka kufahamu kiasi cha fedha ambacho Serikali imewalipa ama kukataa kuwalipa wazabuni na wakandarasi wa ndani baada ya kuwasilisha madai yao na kufanyiwa uhakiki.

TANZANIA YASISITIZA MPANGO WA MATTEI UZINGATIE MAHITAJI STAHIKI YA AFRIKA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Italia. Katika Mkutano huo, Mhe. Makamba anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Italia. Katika Mkutano huo, Mhe. Makamba anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Viongozi mbalimbali walioshriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Italia wakiwa katika picha ya pamoja.


WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Mhe. January Makamba (Mb.) ambaye anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Italia amesisitiza umuhimu wa mpango wa Mattei kuzingatia mahitaji sahihi ya Afrika ili uweze kuleta matokeo stahiki barani Afrika.

Tuesday, January 30, 2024

RAIS SAMIA AZINDUA UGAWAJI WA VIZIMBA VYA KUFUGIA SAMAKI NA BOTI ZA KISASA KWA AJILI YA WAVUVI WA KANDA YA ZIWA, JIJINI MWANZA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa vizimba vya kufugia Samaki na Boti za Kisasa kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024. Wengine katika picha ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emanuel Nchimbi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos Makalla, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Riziki Shemdoe pamoja na viongozi wengine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mkoa wa Mwanza mara baada ya uzinduzi wa ugawaji wa Boti za Kisasa na vizimba kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa katika uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos Makalla mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa ajili ya ziara ya Kikazi ya siku moja tarehe 30 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel Nchimbi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa ajili ya ziara ya Kikazi ya siku moja mkoani humo tarehe 30 Januari, 2024.

WAJUMBE TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI WATEMBELEA MAONESHO YA WIKI YA SHERIA DODOMA


Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk leo Januari 29,2024 wametembelea maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. Maonesho ya Wiki ya Sheria yalianza Januari 24, 2024 na yamataraji kufikia tamati Januari 30,2024.
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume,Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk leo Januari 29,2024 wametembelea maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. Maonesho ya Wiki ya Sheria yalianza Januari 24, 2024 na yamataraji kufikia tamati Januari 30,2024.
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume,Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk leo Januari 29,2024 wametembelea maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. Maonesho ya Wiki ya Sheria yalianza Januari 24, 2024 na yamataraji kufikia tamati Januari 30,2024.

WAZIRI KAIRUKI ATOA MAAGIZO MAZITO KWA TANAPA KWENYE UAPICHO WA KAMISHINA KUJI


Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki ametoa maelekezo mazito kwa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kulitaka libadilike ili liweze kuchangia ipasavyo kwenye uchumi wa taifa kuipitia utalii na kuhifadhi raslimali kwa faida ya kizazi cha sasa na baadaye.

Mhe. Kairuki ametoa maelekezo hayo leo Januari 29,2024 kwenye hafla ya uvalishaji cheo na uapisho wa Kamishna wa uhifadhi,Musa Kuji katika makao makuu ya TANAPA jijini Arusha.
Amesisitiza kuwa katika kipindi hiki TANAPA linatakiwa kuja na ubunifu wa hali ya juu katika kutangaza vivutio vya utalii na kubaini mazao mapya ya utalii ili sekta ya utalii iweze kufikia lengo la Ilani ya Chama Cha mapinduzi (CCM) ya kuwa na wageni milioni tano na kuliingizia taifa jumla ya dola za kimarekani bilioni sita ifikapo mwaka 2025.

Amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa maono yake ya kuifungua Tanzania duniani kupitia Filamu ya The Royal Tour na kuwataka watumishi wa wizara yake kuchapa kazi ili kuenzi kwa vitendo maono ya Rais.

KAMISHNA GENERALI WA DAWA ZA KULEVYA AIPONGEZA OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI


Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo (Kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi jinai David Elias kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali aliyekua akimpa maelezo wakati Kamishna huyo alipitembelea Banda la Mkemia Mkuu katika maonesho ya Wiki ya Sheria Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi jinai David Elias kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali aliyekua akimpa maelezo wakati Kamishna huyo alipitembelea Banda la Mkemia Mkuu katika maonesho ya Wiki ya Sheria Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.

Na Sylvester omary, Dodoma
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo, ameipongeza Mamlaka ya Maabara ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa utoaji wa haraka wa ripoti za uchunguzi na uboreshaji wa mifumo ya utendaji kazi.

Kamishna Jenerali ameyasema hayo leo jijini Dodoma alipotembelea banda la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwenye maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square.
 

AMUUNGUZA KWA MAFUTA YA MOTO JIRANI KISA KWANINI AMEIGA KUSUKA MTINDO WAKE WA NYWELE


Mkazi wa Nairobi, nchini Kenya amemmwagia mafuta ya kukaangia samaki jirani yake kwa madai ya kumuiga kusuka mtindo wa nywele.

Mkazi huyo aliyetambulika kwa jina la Catherine Wanjiru, amedaiwa kummwagia mafuta yaliyochemka, Sherry Nyanchomba, kisha kumtengua taya na kuvunja meno.

Tukio hilo limetokea Januari 16, 2024 kwenye makazi yao huko Dandora, Nairobi, hii ni kwa mujibu wa Tovuti ya Citizen ya nchini humo.

Inaelezwa kwamba Nyanchomba alikuwa akirejea nyumbani usiku ndipo alipokutana na Wanjiru mlangoni ambapo alimshutumu kumuiga mtindo wake wa nywele.

Baada ya kumshutumu inaelezwa Wanjiru alikwenda kuchota mafuta ya moto yaliyokuwa karibu na kudaiwa kuyamimina usoni kwa Nyanchomba kabla ya kuanza kupigana.

WAZIRI MBARAWA AITAKA TANROADS KUSIMAMIA JENGO LA ABIRIA TABORA


Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akikagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Tabora.
Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Tabora, jengo hilo litakapokamilika litakuwa na uwezo na kuhudumia abiria takribani 120 kwa wakati mmoja.
Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi, Dkt. Batlida Burian, wakati Waziri huyo alipomtembelea Mkuu wa Mkoa huyo ofisini kwake Mkoani Tabora.
PICHA NA WIZARA YA UCHUKUZI


WAZIRI wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa ameutaka Wakala wa Barabara (TANROADS) kuhakikisha mradi wa Jengo la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Tabora unaotekelezwa na Mkandarasi wa Kampuni ya M/s Beijing Construction Enginerring Group CO. Ltd unakamilika ndani ya muda atakaoongezwa.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo Mkoani humo Waziri Prof. Mbarawa amesema pamoja na changamoto zilizojitokeza tayari Serikali imechukua hatua stahiki ili kuhakikisha mradi huo unakamilishwa ili kuiunganisha Tabora na mikoa mingine kwa njia ya usafiri wa anga..

VETA SINGIDA YAISHUKURU EWURA KWA MAFUNZO


Mhandisi Mwandamizi wa Umeme EWURA Kanda ya Kati, Nicholaus Kayombo (kushoto) akiwaelekeza wanafunzi wa VETA Singida namna ya kufanya maombi ya leseni kwa mfumo wa LOIS wakati wa mafunzo yaliyotolewa na EWURA chuoni hapo, leo 29 Jan 2024.
Wanafunzi wakifuatilia kwa umakini mafunzo kutoka kwa Wataalam wa EWURA juu ya udhibiti wa sekta ya umeme hususani masuala ya leseni leo, 29 .01. 24 katika chuo cha VETA Singida.

UWT ZANZIBAR YAMPONGEZA DKT MWINYI KWA KUONGEZA IDADI YA WANAWAKE KATIKA SAFU YA VIONGOZI


Naibu Katibu Mkuu wa UWT Ofisi Zanzibar Tunu Juma Kondo akitoa pongezi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi kufuatia uteuzi alioufanya january 27 mwaka huu, ulioongeza idadi ya Wanawake katika nafasi za Uongozi ,hafla ilyofanyika afisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
Katibu wa UWT Mkoa wa Kusini Unguja Zuwena Suleiman Mohamed akichangia wakati wa hafla ya kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa kuongeza idadi ya wanawake katika safu ya Uongozi katika Uteuzi alioufanya January 27 mwaka huu,huko Ofisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR

Umoja wa Wanawake (UWT) Ofisi ya Zanzibar umempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapunduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuongeza idadi ya Wanawake katika safu ya Uongozi.

Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo Tunu Juma Kondo katika kikao cha pamoja,kilichowashirikishi Viongozi wa UWT Zanzibar na kufanyika Ofisi kuu ya CCM Kisiwanduwi Wilaya ya Mjini.

WAMILIKI WA VYOMBO VYA USAFIRI WAPATIWA ELIMU KUJIKWAMUA NA UMASIKINI


Mamlaka ya udhibiti Usafiri Ardhini LATRA imetoa elimu kwa wamiliki wa Vyombo vya moto ikiwemo daladala na bajaji juu ya umuhimu wa kuwa na ushirika wao wa pamoja ama kuwa na kampuni ambayo itakua inatetea maslahi yao.

Meneja wa Leseni wa Mamlaka hiyo Bwana Leo Ngowi wakati akizungumza na wamiliki wa daladala na Bajaji Jijini Arusha leo Januari 29, 2024 amesema kuna umuhimu wa wamiliki hao kuanzisha ushirika wao ama kuwa na kampuni ambayo lengo lake litakua ni kuboresha huduma ya usafirishaji lakini pia wao wenyewe kujiimarisha kiuchumi.

Bwana Ngowi ameendelea kubainisha kuwa washiriki katika semina hiyo walipata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo faida za kuwa na umoja huo ambao kama ukifanikiwa kuanzishwa utasaidia kuwa na mfumo wa kisasa ukilinganisha na mfumo wa sasa ambao unatumika usiokidhi viwango.
Halikadhalika amesema kuwa baada ya Kuanzishwa kwa Chama hicho cha ushirika huduma za usafirishaji katika Jiji hilo zitaimairika na kuboreka kwa kiasi kikubwa.

Monday, January 29, 2024

WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA ITALIA




Waziri Mkuu wa Italia, Mhe. Giorgia Meloni akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) katika ukumbi wa mkutano jijini Roma, Italia.

Waziri Makamba yupo Roma kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Nne wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Italia ulioanza tarehe 28 - 29 Januari 2024.

MAWAZIRI WA NISHATI TANZANIA, ZAMBIA WAJADILI UJENZI WA BOMBA JIPYA LA MAFUTA


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko pamoja na Waziri wa Masuala ya Nishati wa Zambia, Mhe. Peter Kapala leo wamefanya kikao kilicholenga kujadili nia ya Serikali ya Tanzania na Zambia kuanza ujenzi wa bomba la inchi 24 la kusafirisha mafuta safi kutoka Tanzania kwenda Zambia.
Kikao hicho kimefanyika tarehe 29 Januari, 2024 jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga, Makatibu Wakuu wa Wizara za Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, (Tanzania) na Dkt. Chisangano Zyambo (Zambia) pamoja na watendaji mbalimbali kutoka Wizara hizo na Mashirika yanayosimamia Mafuta.
Dkt. Biteko amesema, majadiliano hayo ya Mawaziri yanatokana na ziara ya Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoifanya nchini Zambia mwezi Oktoba mwaka 2023 ambapo katika mazungumzo yake na Rais wa Zambia, Mhe. Haikande Hichilema walijadiliana kuhusu kuongeza uwekezaji kwenye Bomba la Mafuta la TAZAMA kwani bomba hilo kwa sasa halikidhi mahitaji kutokana na kuwa na ukubwa wa inchi 12.

“Kulingana na maendeleo makubwa katika nchi zetu mbili, mahitaji ya mafuta yamekuwa makubwa ndio maana inabidi kujenga bomba jingine jipya kubwa ambalo litasafirisha mafuta kutoka Tanzania kwani kuna Bandari, bomba hili litakalojengwa pembeni ya Bomba la Mafuta la TAZAMA litasafirisha mafuta pia kwenda mikoa ya kusini mwa Tanzania na hivyo kupunguza gharama za usafirishaji na kuwapatia wananchi mafuta ya gharama nafuu.” Amesema Dkt. Biteko.

UTOAJI HATI ZA UMILIKI ARIDHI WASITISHWA ARUSHA,NI UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA WAZIRI WA ARIDHI



Na Mwandishi Wetu, Arusha

KAMISHNA wa Ardhi Mkoa Arusha, Geofrey Msomsojo amezuia zoezi la utoaji hati za umiliki wa ardhi, katika eneo la ekari sita, lililopo kata ya Olmoti katika jiji hilo kutokana na eneo hilo kuwa na mgogoro kwa miaka 17 sasa, ikiwa ni utekelezaji agizo la siku 30 la Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Slaa.

Waziri Slaa wiki iliyopita, alitembelea eneo hilo na kuzungumza na William Mollel ambaye analalamika eneo lake kuvamiwa pamoja na majirani wa eneo.

Katika mgogoro huo, familia ya Mollel inamtuhumu aliyekuwa Ofisa Ardhi jiji la Arusha, Chritopher Kitundu ambaye hivi sasa amehamishiwa wilaya ya Tandahimba kuuziwa eneo na Leah Neeva hilo kinyume cha sheria.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Kitundu alikana kuvamia eneo hilo na kueleza wanaomlalamikia waende mahakamani badala ya kumtuhumu kuvamia eneo lao.

“Mimi sijavamia eneo la mtu, kama kuna wanaonilalamikia basi waende mahakamani, ndipo haki inaweza kupatikana,” amesema.

TANZANIA KUNUFAIKA NA MIRADI YA MPANGO WA MATTEI (TANZANIA TO BENEFIT FROM MATTEI PLAN PROJECTS)


Tanzania imechaguliwa kuwa moja ya nchi nane za Afrika zitakazopewa kipaumbele na Italia kupitia mpango mpya wa kimkakati wa Mattei (Mattei Plan) ambapo kiasi cha Euro bilioni 5 za awali kimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.\n\nMiradi hiyo ya kipaumbele kupitia Mpango mpya wa Kimkakati wa Mattei (Mattei plan) ipo katika sekta ya nishati, elimu na kilimo.
 
Taarifa hiyo imetolewa na Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wa Italia, Mhandisi Alfredo Cestari alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) pembezoni mwa Mkutano wa Nne wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Italia unaendelea Roma, Italia. 
Mhandisi Cestari alieleza kuwa utekelezaji wa mpango huo utaanza mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika na Italia, ambapo Serikali ya nchi hiyo itafadhili miradi ya kipaumbele kwa nchi nane za awali za Afrika. Hatua hiyo itahusisha pia kugharamia gharama za upembuzi yakinifu ya miradi itakayopendekezwa. 

Kama hatua ya utekelezaji ya mpango huo, ujumbe wa wataalam kutoka Chemba ya Biashara ya Italia ikiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Mhe. Dkt. Edmondo Cirielli unatarajiwa kuwasili nchini Tanzania ndani ya mwezi mmoja kwa ajili ya kukutana na timu ya wataalam ya upande wa Tanzania kwa ajili ya kukamilisha hatua za awali za utiaji saini wa ushirikiano huo wa pande mbili utakaohusisha utekelezaji wa miradi itakayopitishwa na pande mbili.

TPA YAIKABIDHI KAMPUNI YA ANOVA CONSULTING ENEO ITAKAPOJENGA BANDARI MBAMBA BAY


Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA ) tarehe 27 Januari,2024 imeikabidhi rasmi kampuni ya Anova Consulting Company ltd eneo itakapojengwa Bandari ya Mbamba Bay iliyopo Wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Meneja wa Bandari za Ziwa Nyasa Bw.Manga Gassaya amesema kampuni hiyo itasimamia ujenzi wa Bandari hii ili kuhakikisha kila kitu kinafanyika katika viwango na kukamilika kwa muda uliokubaliwa katika mkataba.

Aidha amesema kuwa kinachofanyika ni kumuonyesha msimamizi wa mradi (Anova Consult) mipaka ya eneo la ujenzi.

Makabidhiano hayo ni kufuatia mkataba wa usanifu na ujenzi wa uendelezaji wa Bandari ya Mbamba Bay uliosainiwa disemba 4,mwaka jana ambapo kampuni ya Xiamen Ongoing Construction Group Co ltd ndio itaendeleza ujenzi wa Bandari hiyo.

MELI 13 ZINAHUDUMIWA MUDA HUU BANDARI YA DAR ES SALAAM


 

*Hizi hapa dondoo 15 muhimu za kuzingatia dhidi ya propaganda hasi kwa bandari ya DSM

1.Magati yote 12 pamoja na maeneo ya kuhudumia shehena za mafuta yanahudumia meli hadi kufikia muda huu wa leo tarehe 28 Januari 2024, tofauti na wapotoshaji wanaoposha kwa makusudi kuwa ni magati mawili (2) tu ndio yanayofanya kazi kati ya magati 12 yaliyopo.

2.Taarifa zinaonesha ukweli halisi watu wakichapa kazi katika magati yote 12 na kuongeza ufanisi. Kwa mfano, Gati namba Sifuri (0) ambalo ni mahsusi kwa kushusha shehena ya magari nalo linahudumia meli MV Yangze 32 ya mizigo mchanganyiko.

3. Idadi na wingi wa meli bandarini unabadilika ukiona leo foleni meli 20 na keshokutwa ukaona meli 20 haina maana ni zilezile maana yake kuna meli zimehudumiwa na nyingine zimekuja kutaka kuhudumiwa.

4. Ni sawa na shuleni mtu anaweza kuhoji mbona kila mwaka shule zinakuwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne. Maana yake ni kuwa kadri wengine wanavyomaliza shule ndivyo wengine wanaanza shule, wa kidato cha nne akimaliza wa kidato cha tatu anapanda cha nne, wa cha pili anapanda cha tatu, wa cha kwanza anapanda cha pili na aliyemaliza shule ya msingi anapanda cha kwanza ni mzunguko. Ndivyo mzunguko wa meli unavyokuwa