Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo taifa Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba chama hicho kinalenga kufikisha mawazo mbadala kwa watanzania kwa dhamira ya kuunga nguvu za pamoja ili kusaidia kujenga nchi kimaendeleo.
Mhe. Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameyasema hayo alipokutana na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Kigoma Mhasham Joseph R. Mlola ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika Mkoani huo ikiwa ni maadhimisho ya chama hicho kutimia miaka kumi tangu kuanzishwa kwake .
Amesema kwamba kufanya hivyo ndio kutekeleza ipasavyo kazi ya vyama vya siasa ambapo msingi wake mkuu ni kuumarisha kidemokrasia kwa kuwa chama hicho hakiamini kwamba siasa ni mapambano bali kinaamini ni namna bora ya kuweza kuwafikia watu na kuweza kushauriana kwa mashirikiano juu ya namna bora ya kuleta mabadiliko .
Aidha amefahamisha kwamba msingi mwengine unaotumiwa na chama hicho ni kuendeleza kukosoa kistaarabu kwani kufanya hivyo hakuhitaji lugha ya kukirihisha bali ni kujenga usawishi kwa watu na kuweza kukubalika.
Akizungunzia suala la Katiba Mpya Mhe. Othman amesema kwamba jambo hilo ni muhimu kuwepo chombo cha mawazo shirikishi ambalo ni Bunge lakini Bunge lililopo sasa lina uwakilishi sahihi wa wananchi kutokana na kutokuwepo uchaguzi huru na wa haki.
Hata hivyo, amesema kwamba Viongozi na Taasisi za dini zinanafasi muhimu katika kujenga Imani kwa wananchi na kuweza kufikia malengo yanayokusudiwa na taasisi za vyama vya siasa.
Akizununzia suala la Serikali ya Umoja wa Kitaifa Mhe. Othman amesema kwamba chama chake akioni furaha wala fahari ya kutananza kujitoa lakini kinalazimika kufanya ivyo kutokana na mazingira ya kutokuwepo dhamira ya kweli kama masarti ya kuingia kwenye serikali hiyo jambo ambalo halikuwa rahisi.
Alisema kwamba Chama chake kipo tayari na kinakaribisha ushauri na maelekezo kutoka kwa viongozi na taasisi za dini mbali mbali pale inapoonekana kwamba kuna mambo hayaendi vyema kwa nia ya kuleta umoja kwenye ujenzi wa nchi.
Naye Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma Mhasham Josep R. Mlola amekipongeza chama hico kwa kuweza kujijenga na kusambaa nchi nzima katika kipindi kifupi cha miaka kumi tokea kuanziswa kwake.
Amekitaka kuendelea kujitaidi kuwa sauti ya wasionasauti kuwatetea watu wa Tanzania na kwamba ni muhimu kutumia mbinu ya mazungunzo katika kufikia vyema maleno na matarajio ya wananchi kupitia majukwaa ya siasa.
Mhe. Othman yupo Mkoani Kigoma kuendelea na ziara yake ya kuadimisa miaka kumi tokea kuanzishwa kwa chama hicho na anatarajiwa kumaliza ziara yake katika Mkoa wa Tabora baadae wiki hii.
Imetolewa na ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo chake cha habari leo tarehe 07.05.04.
No comments:
Post a Comment