ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 8, 2024

SHUGHULI ZA KIUCHUMI ZIENDE SAMBAMBA NA MALEZI BORA YA WATOTO WETU

Wafanyabiasha wa Kijiji cha Lumbila Kata ya Ruanda Wilayani Mbozi, wametakiwa kuimalisha malezi kwa watoto wao na sio kuwaachia ndugu, majirani au wasaidizi wa kazi jukumu hilo.

Akizungumza wakati akitoa elimu ya umuhimu wa malezi bora kwa watoto katika ukumbi wa kijiji hicho Mei 08, 2024 Polisi Kata wa Kata ya Ruanda Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Happy Lumbe alisema, endapo malezi ya watoto yataimalishwa na kusimamiwa vyema ni wazi kuwa hakuta kuwa na mmomonyoko wa maadili utakaochangia watoto kutofikia malengo ya kielimu na maisha yao ya baadae.
"Ili kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto ni lazima kuimalisha malezi bora kwa watoto wetu ikiwa ni pamoja na kufuatilia mabadiriko ya tabia zao" alisema Mkaguzi Lumbe.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao Jobajoba Yusuph mbali ya kupongeza jitihada mbalimbali za Jeshi la Polisi katika kuyafikia makundi yote katika jamii aliahidi kuwafikishia ujumbe huo wafanyabiashara wenzake wasiofika kwenye kikao hicho kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao watapata ujumbe huo kupitia vikao

No comments: