Advertisements

Sunday, June 16, 2024

WATOTO WAPATE MALEZI BORA YENYE MAADILI: RAIS SAMIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisherehekea Siku ya Mtoto wa Afrika akiwa pamoja na wajukuu, Ikulu jijini Dar es Salaam. Siku hii huadhimishwa Juni 16 ya kila mwaka.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amejumuika na wajukuu toka maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika kwenye viwanja vya Ikulu Juni 16, 2024

Amesisitiza umuhimu wa Serikali, familia na jamii kushirikiana kuhakikisha watoto wanapata malezi bora yenye maadili mema, na kuhakikisha usalama wa mtoto ni jukumu la jamii nzima na siyo mzazi tu, vilevile kuwapatia elimu na historia za kuwahimiza uzalendo kwa nchi yao tangu wakiwa wadogo.
“Ndoto na matarajio ya watoto katika kila kona ya nchi yetu viendelee kutukumbusha jukumu la kila mmoja wetu katika kazi ya kujenga taifa bora kwa kuunda na kutekeleza sera sahihi, ikiwemo uwekezaji mkubwa tunaoendelea kuufanya katika sekta za elimu na afya. Tuendelee kuifanya kazi hii sambamba na ile ya kutunza amani, umoja na mshikamano wa nchi yetu, kwani uhakika wa kesho yao ndio uhakika wa uimara, usalama na ustawi wa nchi yetu.” Amehitimisha Rais Samia katika ujumbe aluouandika kwenye mitandao ya kijamii.









No comments: