Sunday, July 14, 2024

GOLDEN WOMEN WASHAURIWA KUENDELEA KUWAFIKIA WAHITAJI


Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akikabidhi zawadi kwa Mkuu wa Kituo cha Huduma cha SAFAAD, Bw. Adolph Alfred, kwa niaba ya Kikundi cha Umoja wa Wanawake wa Wizara ya Fedha (Golden Women) walipotembelea kituo hicho na kutoa mahitaji mbalimbali, kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake tarehe 14 Julai, 2024.
Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Fedha , Bi. Jenifa Christian Omolo (wapili kulia), akizungumza na baadhi ya Watoto, Frolentina Aloyse (watatu kulia) na Sharifa Sungura (wanne kulia), wanaolelewa katika Kituo cha Huduma cha SAFAAD, kilichopo Chamwino mkoani Dodoma baada ya kutembelea kituo hicho.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo (wakwanza kushoto), akiteta jambo na viongozi wa Kikundi cha Umoja wa Wanawake wa Wizara ya Fedha (Golden Women), walipotembelea Kituo cha Huduma cha SAFAAD, kilichopo Chamwino mkoani Dodoma, katikati ni Mwenyekiti wa Golden Women Bi. Consolatha Maimu na Katibu wa kikundi hicho Bi. Nyanzala Nkinga.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akizungumza na baadhi ya watumishi wanawake wa Wizara ya Fedha, Wamiliki wa Kituo cha Huduma cha SAFAAD, walezi na watoto wanaolelewa katika kituo hicho, kilichopo Chamwino Mkoani Dodoma baada ya kutembelea na kutoa mahitaji mbalimbali ikiwemo vyakula, vinywaji, nguo, fedha taslim na mahitaji mengine.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo (wakwanza kulia), akizungumza na Viongozi wa Kituo cha Huduma cha SAFAAD, kilichopo Chamwino mkoani Dodoma, baada ya kutembelea kituo hicho, wakwanza kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Huduma cha SAFAAD, Bw. Adolph Alfred pamoja na Bi. Joan Abdallah.

Na: Josephine Majura na Asia Singano WF, Dodoma.

Umoja wa Wanawake wa Wizara ya Fedha, (Golden Women), wameshauriwa kuendeleza utamaduni wa kutoa misaada mbalimbali kwa watu wenye mahitaji maalumu ili kuwasaidia kufikia malengo yao.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi Jenifa Christian Omolo, ametoa ushauri huo alipotembelea Kituo cha Huduma cha SAFAAD, kilichopo Kijiji cha Membe, Wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Aliongeza kuwa kuwakumbuka watu wenye mahitaji mbalimbali ni jambo zuri hivyo ni vema utaratibu huo ukaendelea ili kuhakikisha wanawafikia makundi mbalimbali ya watu wenye uhitaji.

"Niwapongeze Uongozi wa Golden Women kwa umoja wenu wa kujitoa kwa hali na mali na kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa”alisema Bi. Omolo

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wizara ya Fedha Bi. Consolatha Maimu, aliahidi kuendelea kuwahamasisha Wanakikundi hao kuwa na utaratibu wa kuwasaidia watu wenye mahitaji mbalimbali.

Naye Mkuu wa Kituo cha Huduma cha SAFAAD, Bw. Adolph Alfred, aliwashukuru Wanawake wa Kikundi cha Golden Women kwa kufika Kituoni hapo na kupeleka mahitaji

Naye mmoja wa wanufaika wa mahitaji hayo Bi. Florentina Aloyce, aliuomba uongozi wa Kikundi cha Golden Women, kuendelea kuwa mabalozi kwa vikundi vingine ili viweze kufika kituoni hapo ili waweze kupata mahitaji kwa kuwa bado wana mahitaji mengi.

Katika kuelekea maadhimisho ya sherehe ya Umoja wa Wanawake, Wizara ya Fedha, imetembelea Kituo cha Huduma cha SAFAAD kwa ajili ya kupeleka mahitaji ikiwemo mahitaji ya shule, vyakula, vinywaji na mahitaji mengine mbalimbali.

No comments: