Saturday, July 13, 2024

MIRADI YA BILIONI 149.5 KUFIKIWA NA MWENGE WA UHURU MANYARA


Na John Walter-Manyara

Mwenge wa uhuru umeingia katika mkoa wa Manyara leo Julai 12,2024 ukitokea mkoani Singida ambapo utakimbizwa Katika Halmashauri zote saba za wilaya tano za mkoa huo.

Mwenge huo utakimbizwa kilomita 980.5 kukagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi 57 ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni 149.5.

Akipokea Mwenge wa uhuru katika kata ya viwanja vya shule ya Sekondari Mwahu kata ya Gehandu Wilayani Hanang' kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Sindida Halina Ndedego, Mkuu wa mkoa wa Manyara Mheshimiwa Queen Sendiga amesema kati ya miradi hiyo, shilingi milioni 837 ni michango ya Wananchi na milioni 500 ni michango kutoka wadau wa Maendeleo.

Amesema miradi 17 yenye thamani ya shilingi Bilioni 134.1 itawekewa mawe ya msingi, miradi 8 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.4 itazinduliwa, miradi minne yenye thamani ya shilingi 1.3 itakaguliwa na kuonwa na kutembelea miradi 28 ya yenye tamani ya shilingi milioni 10.7.

Sendiga amesema kati ya fedha hizo nguvu za wananchi ni shilingi milioni 102.5, serikali bilioni 72.8, Halmashauri shilingi Milioni 169.7 wadau wa Maendeleo shilingi Milioni 76.5.0

Baada ya kuupokea Mwenge wa Uhuru, Sendiga amekabidhi Mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa wilaya ya Hanang' Almishi Hazali ambapo umekimbizwa kilomita 130 na kutembelea miradi 9 yenye thamani ya shilingi bilioni 12.522.

Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amesema serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwatumikia Wananchi kwa kutoa fedha nyingi kwenye miradi hivyo wasimamizi wawe makini ili fedha hizo zitumike kama ilivyokusudiwa.

Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 unaongozwa na kaulimbiu isemayo Tunza Mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa Ujenzi wa taifa endelevu.

No comments: