Saturday, July 13, 2024

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI ALHAJJ DK.HUSSEIN ALI MWINYI AMEJUMUIKA NA WANANCHI WA KILIMA KATIKA IBADA YA SALA YA IJUMAA



RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Waumini wa Dini ya Kiislam, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Ijumaa iliyofanyika leo 12-7-2024 katika Msikiti wa Kilimani Wilaya ya Mjini Unguja.





RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam, katika kuitikia dua ikisomwa na Sheikh.Shariff Abdulrahaman Muhidin (hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa dua maalumu, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti wa Kilimani Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 12-7-2024 na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi na Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar Mhe.Toufiq Salim Turky na (kushoto kwa Rais) Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar Sheikh.Khalid Ali Mfaume

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Wananchi baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti wa Kilimani Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 12-7-2024

No comments: