ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 18, 2024

ZANZIBAR INA WAJASIRIAMALI VIJANA WENGI WENYE VIPAJI WANAOCHIPUKIA KWENUE UJASIARIAMALI


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akielekea katika ukumbi wa mkutano katika Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Zanzibar, kwa ajili ya ufungua Mkutano wa Tatu wa Pamoja Kati ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar na Kituo cha Utafiti za Maendeleo ya Kijamii, Uchumi na Uchambuzi wa Sera Zanzibar (ZRCP) na (kushoto kwa Rais)Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar.Mhe Dkt. Saada Mkuya Salum na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, uliofanyka leo 17-9-2024.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akihutubia na kuufungua Mkutano wa Tatu wa pamoja Kati ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar na Kituo cha Utafiti za Maendeleo ya Kijamii, Uchumi na Uchambuzi wa Sera Zanzibar (ZRCP) uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 17-9-2024.

WASHIRIKI wa Mkutano wa Tatu wa Kituo cha Utafiti za Maendeleo ya Kijamii, Uchumi na Uchambuzi wa Sera Zanzibar (ZRCP) kwa kushirikiana na Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na kuufungua mkutano huo, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 17-9-2024, kuzungumzia “Matumizi ya Teknolojia katika kuongeza ubunifu ili kuweza kuchokea uazishaji wa Taasisi changa na zinazoinukia

WASHIRIKI wa Mkutano wa Tatu wa Kituo cha Utafiti za Maendeleo ya Kijamii, Uchumi na Uchambuzi wa Sera Zanzibar (ZRCP) kwa kushirikiana na Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na kuufungua mkutano huo, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 17-9-2024, kuzungumzia “Matumizi ya Teknolojia katika kuongeza ubunifu ili kuweza kuchokea uazishaji wa Taasisi changa na zinazoinukia

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Ripoti ya Utafiti wa Wazalishaji Wanaoibuka Zanzibar, akikabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Utafiti za Maendeleo ya Kijamii, Uchumi na Uchambuzi wa Sera Zanzibar (ZRCP) Prof Mohammed Hafidh Khalfan, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Tatu wa Kituo cha Utafiti Masuala ya Kijamii Zanzibar (ZRCP) uliyofanyika leo 17-9-2024 katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akikabiwa zawadi maalumu na Mjumbe wa Bodi ya Kituo cha Utafiti za Maendeleo ya Kijamii, Uchumi na Uchambuzi wa Sera Zanzibar (ZRCP) Bi.Rukiya Wadoud (kulia) wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa Tatu wa Kituo hicho uliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Zanzibar leo 17-9-2024


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema, Zanzibar ina kila sababu ya kuanzisha mfumo wezeshi kwenye biashara zinazochipukia zenye uwezo wa kukua kwa haraka ili kustawisha maisha ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipofungua mkutano wa tatu wa pamoja wa taasisi ya Utafiti na Uchambuzi wa Sera za Kijamii na Uchumi Zanzibar, (ZRCP) leo tarehe 17 Septemba, 2024 kwenye ukumbi wa hoteli ya Madinatul Bahri, Wilaya ya Magharibi B.

Amefahamisha kuwa Zanzibar ina wajasiriamali vijana wenye vipaji wanaochipukia kwenye ujasiriamali, hivyo ni muhimu kuwakuza kwaajili ya uchumi jumuishi na endelevu wa Taifa.

Pia Dk. Mwinyi alisema, kuna umuhimu mkubwa wa kuwawekea mazingira bora na rafiki ili wavumbue biashara zenye faida kubwa na kuviendeleza vipaji vyao kwa maslahi mapana ya Taifa.

Alifahamisha, nchi nyingi duniani zikiwemo Uholanzi, India, Korea Kusini pamoja na nchi za Afrika kama Kenya, Tunisia, Afrika ya Kusini na Nigeria zimetumia mfumo huo ipasavyo katika kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii, kukuza utajiri wa nchi zao, kuongeza pato la taifa na kutengeneza ajira zenye maslahi makubwa.

Rais Dk. Mwinyi amezielekeza taasisi zilizoratibu mkutano huo, kuongoza mijadala na mada zitakazojadiliwa kwa umakini ili ziletee tija nchini kulingana na mazingira ya kiuchumi na biashara ya Zanzibar.

Aliwahakikishia wadau na washiriki wa mkutano huo kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kuziimarisha Taasisi za kukuza Uchumi ili kuhakikisha vijana wanakuza taaluma zao na kushiriki kikamilifu katika kuvumbua na kuendeleza vipaji vyao.

Halikadhalika Rais Dk. Mwinyi alitoa wito kwa taasisi za Serikali kuzitekeleza kwa vitendo sera na miongozo mbalimbali itakayoanzishwa na ile iliyopo yenye lengo la kusimamia utekelezaji wa maazimio ya kukuza vipaji vya wataalamu kupitia nyanja zote za ubunifu na teknolojia.

Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Dk. Saada Mkuya Salum amesema utafiti unofavywa na kituo cha ZRCP unalengo la kuweka msukumo wa kufanikisha malengo ya Serikali na kuleta mageuzi kwa kiasi kikubwa yanayotokana na sayansi na teknolojia kwa vile Zanzibar inakusudia kuanzisha soko la mitaji hivyo, ni vyema kuwa na namna bora ya kufuatilia matokeo yanayotokana na utafiti ili kufikia malengo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa ZRCP Juma Reli, amesema ZRCP imekusudia kuwa kituo bora chenye kutoa tafiti za hali ya juu na zenye manufaa kwa jamii katika ukanda wa Afrika Mashariki na kuihakikishia Serikali kwamba kituo hicho, kipo tayari kufanyakazi na Serikali kwa weledi, ukweli na uadilifu.

Mkutano huo wa siku mbili imewakutanisha pamoja wadau kutoka taasisi mbalimbali za umma na binafsi, washirika wa maendeleo na taasisi za kimataifa, unalengo la kutafuta na kujadili namna bora ya kutumia teknolojia na utafiti ili kubaini changamoto na mwelekeo mpya wa kuwakuza wajasiriamali wanaochipukia.

No comments: