ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 22, 2024

PINDA AKUTANA NA MABALOZI WA SADC WANAOWAKILISHA NCHI ZAO BOTSWANA


Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, (katikati) akiwa na Balozi wa Angola na Kiongozi wa mabalozi wa SADC nchini Botswana Mhe. Beatriz Morais (kulia) na Balozi wa Tanzania nchini Botswana Mhe. James Bwana (kushoto) alipokutana kuwaarifu juu ya uwepo wa misheni ya uangalizi wa SADC katika uchaguzi Mkuu wa Botswana , jijini Gaborone tarehe 21 Oktoba 2024.

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, (katikati amekaa) akiwa na Mabalozi wa SADC wanaoziwakilisha nci zao nchini Botswana walipokutana jijini Gaborone tarehe 21 Oktoba 2024.

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, amekutana na Mabalozi kutoka nchi za SADC wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana katika kikao kilichofanyika jijini Gaborone tarehe 21 Oktoba 2024.

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Pinda amesema amewaarifu Mabalozi hao juu ya uwepo wake kama Mkuu wa misheni ya Uangalizi ya Uchaguzi ya SADC Pamoja na waangalizi wengine kutoka nchi wanachama wa SADC.

Ameeleza kuwa amekutana nao ikiwa ni sehemu ya ratiba zake mbalimbali ili kuwasiliana nao moja kwa moja na hivyo kusaidia waangalizi kupata picha halisi ya jinsi maandalizi ya uchaguzi huo kwa ujumla yanavyokwenda.

Amesema SEOM imejipanga na iko tayari kutekeleza jukumu lake la Uangalizi kwa ukamilifu kama walivyoaminiwa na Jumuiya na kuwatuma kuifanya kwa niaba yao.

Amesema wao kama viongozi wa SEOM watakuwa na mikutano na watu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kusikiliza na kupata maoni ili kuhakikisha kazi yao ya uangalizi inakwenda vizuri

Akizungumza kwa niaba ya Mabalozi hao Balozi wa Jamhuri ya Angola na Mkuu wa Mabalozi wa SADC nchini Botswana Mheshimiwa Beatriz Morais ameshukuru kukutana na uongozi wa SEOM na kuahidi kushirikiana nao ili kuhakikisha kazi yao ya uangalizi inafanyika kwa mafanikio na hivyo kuleta tija na ufanisi kwa Jumuiya na nchi inayohusika.


No comments: