ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 22, 2024

SILLO AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUBORESHA ELIMU


Naibu waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mbunge wa Jimbo la Babati vijijini Mheshimiwa Daniel Sillo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha nyingi jimboni humo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu ya awali na msingi jambo litakalowawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora na salama.

Mheshimiwa Sillo ametoa Shukrani hizo alipokuwa akizungumza na Wananchi,walimu na Wanafunzi kwenye mahafali ya 16 ya kidato cha nne shule ya Sekondari Duru iliyopo Kijiji cha Endagwe kata ya Duru oktoba 21,2024.

Sillo amesema katika muda wa miaka minne wa awamu ya sita madarakani yamejengwa madarasa mapya, ya zamani yameboreshwa, shule mpya zimejengwa.

Katika hatua nyingine amewataka wazazi na walezi kuendelea kuwahimiza watoto wao kuwa na maadili mema hata baada ya kuhitimu kidato cha nne ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.

Amewasihi kidato cha nne kusoma kwa bidii kwa kushirikiana wao pamoja na walimu wao ili wafanye vizuri katika mitihani ya Mwisho Mwezi Novemba.

No comments: