Afisa wa Program Mafunzo wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Anna Sangai akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi wakati wa ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya uongozi kwa wanawake wagombea Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa vijiji, mitaa na vitongoji iliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Mwezeshaji wa Mafunzo Deo Temba akiwasilisha mada kuhusu dhana za jinsia na ushiriki wa Wanawake katika uongozi kwa washiriki kutoka vyama vya siasa mbalimbali katika warsha ya mafunzo ya uongozi kwa wanawake wagombea Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa vijiji, mitaa na vitongoji iliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wakichangia mada kwenye warsha ya mafunzo ya uongozi kwa wanawake wagombea Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa vijiji, mitaa na vitongoji iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha Wananchi (CUF), ACT Wazalendo, Chama cha Kijamii (CCK) na NCCR Mageuzi wakifuatilia ufunguzi pamoja na mada zilizokuwa zinatolewa wakati wa ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya uongozi kwa wanawake wagombea Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa vijiji, mitaa na vitongoji iliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umefanya mafunzo ya uongozi kwa wanawake wagombea Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa vijiji, mitaa na vitongoji kutoka katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha Wananchi (CUF), ACT Wazalendo, Chama cha Kijamii (CCK) na NCCR Mageuzi ili kutambua masual,a muhimu ya kijinsia katika uongozi.
Mafunzo hayo ni sehemu ya shughuli za TGNP za kila mwaka za kujenga uwezo kwa viongozi wanawake ili kutambua umuhimu wa kuzingatia masuala ya kijinsia katika kutekeleza afua mbalimbali ikiwepo uandaaji wa mipango, miradi ya maendeleo inaytozingatia mahitaji ya kijinsia kwa makundi yote.
Wanawake wanaoshiriki mafunzo haya wanatoka katika kata na halmashauri tofauti ambao wapo kwenye program maalum ya malezi (ukungwi) na ushauri (Mentorship and Coaching) inayolenga kuwajenga kuwa viongozi bora ikiwepo kuwajengea uwezo na ujasiri wa kusimama mbele za watu na kujieleza, ikiwa ni pamoja na kuvunja vikwazo vinavyosababisha ukatili wa kijinsia na kukwamisha ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi na maamuzi.
Akizungumza kwaniaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Mkuu wa Program Mafunzo ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Anna Sangai, amesema lengo kuu la warsha hiyo ili kuongeza uelewa wa dhana ya jinsia na uongozi pamoja na kujenga uelewa wa pamoja kuhusu mifumo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na fursa zilizopo katika kuwezesha wanawake wanashiriki kwenye nafasi za maamuzi.
Pia amesema wanaweka mikakati ya pamoja ya kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi kwenye kata, vijiji, mitaa na vitongoji husika pamoja na kuimarisha mahusiano na kujenga nguvu ya pamoja na kayoka kutekeleza ajenda ya usawa wa kijinsia katika siasa.
Aidha, Anna amesisitiza kwamba, licha ya nafasi za kisiasa zinazogombewa katika uchaguzi wa serikali za Mitaa, pia zipo fursa nyingine za uongozi ambazo wanawake wanaweza kuzishika zikiwepo Kamati, Bodi za afya, elimu, AMCOS na mabaraza ya ardhi ambako ni maeneo muhimu kwa maendeleo yanayohitaji ushiriki wa wanawake.
No comments:
Post a Comment