Friday, November 22, 2024

MKUTANO WA WAJASIRIA MALI KUJADILI CHANGAMOTO NA FURSA ZA UPATIKANAJI MITAJI KWA WAJASIRIA MALI WAFANYIKA ZANZIBAR


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Sharif Ali Sharif akitoa hotuba ya ufunguzi katika hafla ya Mkutano wa Majadiliano kati ya Sekta Binafsi na Serikali kuhusiana na Changamoto na Fursa za Upatikanaji wa Mitaji kwa Vijana Wajasiria mali hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanya Biashara ZNCC Ali Amour akitoa hotuba ya makaribisho kwa Mgeni rasmi katika hafla ya Mkutano wa Majadiliano kati ya Sekta Binafsi na Serikali kuhusiana na Changamoto na Fursa za Upatikanaji wa Mitaji kwa Vijana Wajasiria mali hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Na.Rahma Khamis Maelezo Zanzibar 21/11/2024
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ,Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mhe Sharif Ali Sharif amesema Serikali inaweka mazingira Bora ya biashara ili kuwawezesha vijana kujiajiri.

Ameyasema hayo katika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege wakati akifungua mkutano Kati ya Sekta Binafsi na Serikali wa kukjadili changammoto na Fursa za Upatikanaji wa Mitaji kwa vijana Wajasiriamali wa Zanzibar.

Amesema kuwa Biashara ni Uti wa mgongo hivyo ni vyema vijana kuwa wabunifu na kuchangamkia fursa zilizopo ili kuweza kufanikiwa katika maisha yao.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya Wafanya biashara Hamad Hamad amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kubadilishana uzoefu wa kibiashara ili kuongeza ujunzi zaidi.

Amesema kuwa mradi wa Tanzania Imeimarisha Sekta Binafsi ( Filter future mradi wa vijana kutoka USAD unawawezesha vijana kwani kupitia mradi huo vijana wameweza kufanikiwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Ali Amour amefahamisha kuwa mradi huo umewasaidia vijana kuwainua kiuchumi kwani umenufaisha Biashara 600 wakiwemo wanawake 318 katika Biashara hizo.

Aidha vijana 200 wamepatiwa mafunzo ambayo yamewawezesha kuimarisha Biashara zao, kusaini mikataba tisa na kutoa vijana 30 kushiriki katika maonyesho ya Biashara nane nane.

Akielezea fursa zinazopatika Meneja wa miradi ya Kilimo kutoka Milele Foundation. Fatma Khamis amesema kuwa Milele inafanya kazi katika Sekta tatu ikiwemo sekta ya Elimu ,afya pamoja Uchumi jamii kwani wana miradi ya kuwawezesha wanawake kwa kufanya Biashara ndogo ndogo na kuwapatia elimu ya biashara ili kuwawezesha.

Nae Hashim Iddi Simba kutoka Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (ZEEA) amesema kuwa Kuna kiasi kikubwa Cha fedha za Serikali ambazo bado vijana hawajazifikia na kuwataka vijana hao kuzichangamkia fursa hizo ili kuweza kuzifikia.

Mkutano huo imeandaliwa na Jumuiya ya Wafanyabiashara kupitia mradi wa ImArisha Sekta Binafsi uliofadhiliwa na USAD

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake