Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mcha Hassan Mcha akizungumza na viongozi wa Mamlaka hiyo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Ununuzi na Ugavi yanayotolwa na Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) yanayoendelea jijini Arusha.
Baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakifuatilia uwasilishwaji wa mada mbalimbali wakati wa mafunzo yanayotolewa na PSPTB.
Baadhi ya wasilisha mada kutoka PSPTB wakifuatilia ufunguzi wa Mafunzo kwa viongozi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uliofanywa na Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Mcha Hassan Mcha.
Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Mcha Hassan Mcha (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa viongozi wa TRA.
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mcha Hassan Mcha ameipongeza Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) kwa kuandaa mafunzo ya siku tatu kwa wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kuhusu mabadiliko ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2023 na kanuni zake za mwaka 2024 pamoja na usimamizi wa mikataba ya Ununuzi na Ugavi.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo, Naibu Kamishana Mcha amesema PSPTB imefanya jambo muhimu la kutoa mafunzo hayo kwasababu suala la Ununuzi linajumuisha idara mbalimbali katika Mamlaka hiyo hivyo mafunzo hayo yataweza kuwajengea uwezo wataalamu ili wakiwa wanafanya majukumu yao waweze kuyatekeleza kwa ufanisi mkubwa.
"Mafunzo hayo ni muhimu kwa TRA kutokana na changamoto mbalimbali katika masuala ya Ununuzi na Ugavi." alisema Mcha.
Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma (PSPTB) Bw. Amos Kazinza aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Godfred Mbanyi ameshukuru Mamlaka hiyo kwa kuendelea kuiamini PSPTB katika kuwajengea uwezo watumishi wa TRA.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake