ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 13, 2024

UZINDUZI WA PROGRAMU YA KUKUZA NA KUWALEA WANAFUNZI KWA UWEKEZAJI WAFANYIKA ZANZIBAR.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Sharif Ali Sharif akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara Baada ya Kuwasili katika Uzinduzi wa Programu ya kukuza na kuwalea Wanafunzi kwa Ujasiria Mali (Inqubalion Program for University Students)katika Chuo Kikuu cha Zanzibar(ZU)Tunguu Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Sharif Ali Sharif akisisitiza jambo wakati akitoa Hotuba ya Uzinduzi wa Programu ya kukuza na kuwalea Wanafunzi kwa Ujasiria Mali (INQUBATION PROGRAM FOR UNIVERSITY STUDENTS)katika Chuo Kikuu cha Zanzibar(ZU)Tunguu Zanzibar.
Baadhi ya Wanafunzi waliohudhuria katika Uzinduzi wa Programu ya kukuza na kuwalea Wanafunzi kwa Ujasiria Mali (INQUBATION PROGRAM FOR UNIVERSITY STUDENTS)katika Chuo Kikuu cha Zanzibar(ZU)Tunguu Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZNAIZBAR.12/11/2024.

Na Ali Issa Maelezo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi,Uchumi na Uwekezaji Sharif Ali Sharif amefurahishwa kuona wanafunzi wa elimu ya juu, sekta binafsi na wadau wengine muhimu wanaungana kwa lengo la kukuza uwezo wa vijana wao kupitia ujasiriamali katika vyuo vikuu.

Ameyasema hayo leo huko Chuo Kikuu Tunguu Zanzibar (ZU) wakati wa uzinduzi wa mpango wa kukuza na kulea wanafunzi wa vyuo vikuu Zanzibar (Aqubation programe for university students).

Amesema vijana ndio nguzo kuu ya kujenga uchumi wa Taifa na kuleta maendeleo endelevu hivyo mpango huo ndio kiunganishi sahihi kwani utasaidia kupunguza tatizo ajira na kuweza kujiajiri wenyewe bila ya kutegemea ajira kutoka serikalini.

Alisema mpango huo una nafasi kubwa ya matumizi ya teknolojia katika ulimwengu, hivyo wanafunzi watafunzwa mbinu za ujasiriamali, kubuni bidhaa na huduma mpya na hatimae kuzipeleka sokoni kwa kutumia nyenzo za kidijitali.

Alieleza kuwa hiyo ni fursa adhimu kwa vijana kujenga msingi wa biashara zinazo weza kuchangia moja kwamoja uchumi wa Zanzibar.

Nae Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Kikuu Zanzibar (ZU) Rashid Juma Rashid alishukuru kuzinduliwa kwa mpango huo ukiwa na nia ya kuondoa changamoto ya soko la ajira nchini ambapo kwa sasa wanafunzi watapata matumaini na fursa kusoma masomo ya ujasiriamali na kuweza kujiajiri wenyewe.

Nae Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Juma Burhan Mohmed alisema lengo la mpango huo ni kujenga mfumo endelevu wa ujasiriamali hapa Zanzibar na kuleta mabadiliko chanya.

“Hivi sasa Zanzibar inakabiliwa na vijana wengi wanaomaliza masomo ya juu kwa viwango mbalimbali na kukosa ajira na kushindwa kulipia mosomo, hivyo mpango huo kwa ushirikiano wao utaondoa changomoto hizo”, alifahamisha Mkurugenzi huyo.

Mpango huo ulitiwa sani kati ya Wakala wa Uwezeshaji, Wananchi Kiuchumi (ZEEA), Jumuiya ya wafaanya biashara Zanzibar na Chuo Kikuu Zanzibar (ZU) na kuhudhuria na wadau mbali mbali.

No comments: