Friday, November 22, 2024

WAONGOZA NDEGE WAPONGEZWA KWA UMAHIRI WAO WA UFANISI WA KAZI NCHINI


Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi TCAA Bw. Daniel Malanga aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi akizindua nembo mpya ya Chama cha Waongoza Ndege Tanzania (TATCA) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 44 wa mwaka uliofanyika Novemba 22, 2023 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi TCAA Bw. Daniel Malanga aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw.Salim Msangi akizungumza na wataalam wa Chama cha Waongoza Ndege Tanzania (TATCA) kuhusu namna Mamlaka hiyo ilivyojipanga kuwawezesha waongozaji ndege kufanya kazi kwa weledi na ufanisi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 44 wa mwaka uliofanyika Novemba 22, 2023 jijini Dar es Salaam.
Rais wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA), Merkiory Ndaboya akizungumza kuhusu namna chama hicho kilivyoweza kuwakusanya na kuwaratibu waongoza ndege nchini Tanzania wakati wa kufunguzi wa Mkutano wa 44 wa TATCA uliofunguliwa Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi TCAA Bw. Daniel Malanga aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw.Salim Msangi jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Waongoza ndege Tanzania (TATCA) pamoja na viongozi wa TCAA wakisikiliza hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw.Salim Msangi iliyosomwa Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi TCAA Bw. Daniel Malanga alipokuwa anafungua mkutano mkuu wa 44 wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA) uliofanyika Novemba 22, 2024 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi TCAA Bw. Daniel Malanga aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw.Salim Msangi akitoa zawadi kwa baadhi ya Waongoza Ndege wastaafu kwa kutambua mchango wao wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 44 wa mwaka uliofanyika Novemba 22, 2024 jijini Dar es Salaam.
Mwongozaji Ndege Mwandamizi mstaafu Bw. Mbarouk Hamad (kulia) akitoa neno la shukrani kwa niaba ya waongozaji ndege wastaafu kwa kutambua mchango wao wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 44 wa mwaka uliofanyika Novemba 22, 2024. Kushoto ni mwongozaji ndege Mwandamizi mstaafu Stephen Muhando.
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi TCAA Bw. Daniel Malanga akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wastaafu (walioshika zawadi) pamoja na viongozi wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 44 wa mwaka uliofanyika Novemba 22, 2024 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi TCAA Bw. Daniel Malanga aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw.Salim Msangi akiwa kwenye picha ya pamoja na waongoza ndege Tanzania waliohudhuria mkutano wa 44 wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA) uliofanyika Novemba 22, 2024 jijini Dar es Salaam.

Tanzania imeelezwa kuwa na Wataalam wa kuongoza ndege nchini wenye umahiri mkubwa na kufanya huduma za usafiri wa anga nchini kuimarika na kuwa yenye idadi ndogo ya matukio.

Hayo yalisemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Daniel Malanga wakati akifungua Mkutano wa 44 wa mwaka wa Chama cha Waongoza Ndege Nchini (TATCA), Novemba 22, 2024 jijini Dar es Salaam.

Bw. Malanga aliongeza kuwa umahiri huo unatokana na ukweli kwamba, wataalam hao wanaandaliwa hapa hapa nchini na kuongeza kuwa mbali ya wataalam hao kuwa mahiri pia TCAA imeendelea kuboresha mazingira yao ya kufanyia kazi ikiwemo kufunga mitambo ya kisasa ya radio za sauti inayorahisisha mawasiliano baina ya muongoza ndege na rubani.

Aidha, Bw.Malanga amevutiwa na Kauli Mbiu  ya TATCA ya mwaka huu inayosema ‘Jenga Afya kwa Uongozaji Ndege wa ufanisi’, na kuwataka waongoza ndege hao licha ya kufanya kazi zao kwa umahiri pia wazingatie kulinda afya zao.

Mbali na ufunguzi wa Mkutano huo, Bw. Malanga pia alizindua Nembo mpya ya TATCA ambayo itatumika kutambulisha shughuli mbalimbali za uendeshaji wa chama hicho nchini.

Mkutano huo wa TATCA mbali na kuhudhuriwa na wanachama wa vyama rafiki vya hapa nchini, pia umehudhuriwa na wawakilishi wa vyama vya waongoza ndege kutoka nchi za Kenya, Uganda na Kongo DRC.

Kwa upande wake Raisi wa TATCA, Bw. Merkiory Ndaboya aliishukuru TCAA kwa kuendelea kuviwezesha vyama vya kitaaluma kuendelea kufanya kazi zao pamoja na mikakati ya TCAA ya kufunga mitambo ya kisasa ya kuongozea ndege inayowarahisishia utendaji kazi wao.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake