Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kufungua fursa zaidi za ajira kwa watanzania nje ya nchi.
Aidha, Mhe. Ridhiwani amesema serikali inatekeleza mpango wa kuwaandaa vijana kuwa na ujuzi stahiki unao wawezesha kumudu ushindani kwenye soko la ajira la kimataifa sambamba na kufanya kazi zenye tija.
Mhe. Ridhiwani amebainisha hayo leo Novemba 28, 2024 Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kuwaaga Vijana wa Kitanzania wanaoenda kufanya kazi nchini Saudi Arabia.
Waziri Ridhiwani Kikwete, amebainisha kuwa Serikali imesaini makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya ajira na nchi ya Falme za Kiarabu (UAE), Saudi Arabia, Iran na Qatar kwa lengo la kuongeza fursa zaajira kwa watanzania kwenye nchi hizo.
"Serikali imeweka malengo mahususi ya kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania kutoka 556,065 kwa mwaka 2022 hadi 1,000,000 ifikapo mwaka 2028," amesema
Vile vile, amesema serikali itaendelea kulinda haki na wajibu wa wafanyakazi wa kitanzania nje ya nchi kwa kuhakikisha wanafanya kazi za staha ili kuongeza idadi ya watanzania wanaofanya kazi za kitaaluma.
Sambamba na hayo, ametoa rai kwa Wauguzi wanao kwenda kufanya kazi nchini Saudi Arabia, kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu ili kuaminika na kuiletea heshima nchi yao Tanzania.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake