Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akiondoa pazia na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla akiweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mahakama ya Mkoa wa Kaskazini Pemba, ikiwa ni Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amewataka watendaji wa mahakama Zanzibar kuhakikisha kwamba wanatoa huduma bora kwa wanachi kwa kwenda sambamba na uwekezaji mkubwa wafedha unaofanywa na serikali kwenye sekta hiyo hasa katika suala la miundo mbinu na majengo ya kuleo.
Mhe. Othman ameyasema hayo huko kinyasini wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba alipoweka jiwe la msingi wa jengo jipya la kileo la Mahakama ya Mkoa wa kazikazi Pemba linalojengwa kwa gharama ya Bajeti ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama sehemu ya mkakati wa serikali kuimarisha uduma za utoaji haki kupitia mahakama.
Amefaamisha kwamba ni vyema watendaji wa Chombo hicho kikaimarisha huduma na upatikanaji wa haki kwa wananchi ili maakama iiwe kimbilio lao badala ya kuikimbia kutokana na kukosa Imani na chombo hicho muhimu .
Amesema kwamba mahakama pia zinapaswa kuwa chombo cha kuchunguza matukio ya vifo vya ghafla na mengine ya namna hiyo kwa kuunda tume zenye usimamamizi wa majaji wanaoaminika na jamii ili kuchunguza matukio ya mauaji na ya vifo yanayojitokeza katika maeneo mbali mbali nchini hivi sasa.
Amesema kwamba kufanya hivyo kutajenga imani kubwa wa wananchi na chombo hicho pia kuweza kutimiza malengo ya serikali ya kukimarishia miundombinu zikiwemo za majengo ya ofisi za majaji, mahakimu, makadhi na watendaji weninge kwenye kada hiyo muhimu katika upatikanaji wa haki.
Amesema kwamba jaji mkuu wa Zanzibar anao uwezo na wajibu wa kisheria kusimamia uchunguzi wa kesi na matukio ya mauaji mbali mbali chini ya utaratibu wa kuunda tume itakayosimamiwa na jaji ainayeaminika ndani ya jamii
Adha Mhe. Makamu amewaleza watendaji hao kwamba hadhi ya chombo hico haitakuwepo kwa kuwa na majengo mazuri yaliyojengwa kwa gharama kubwa pekee bali itatokana na namna mahakama katika ngazi mbali mbali zinavyosimamia mashauri mbali mbali na haki ikaweza kupatikana na wananchi kujenga Imani na chombo chao hicho.
Kwa Upande wake Jaji Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdalla amefahamisha kwamba hivi sasa mahakama mbali mbali zimeimairisha na kuarakikisha kusikiliza mashauri mbali mbali na kuweza kumaliza kesi nyingi kwa wakati na kwamba maakama nyingi zimefanikiwa kumaliza mrundikano wa kesi kutokana na juhudi zinazofanywa kuimarishwa.
Amesema kwamba chombo ghicho pia kimefanikiwa kupata mkopo wa dola milioni 30 ambazo zitatumika katika uimarishaji wa makakama awamu inayofuata na kukifanya chombo hicho kuwa na utendaji wa kileo ulioimarika kwa vifaa nba miundombinu ya kisasa lakini na watendaji mahiri wenye utaalamu bora.
Naye Kaimu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba na Sheria Shamata Shaame Khamis amesema kwamba ujenzi wa majengo ya mahakama ni sehemu ya kuemdeleza maboresho muhimu katika chombo hicho kupitia bajeti inayotengwa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuwapatia wananchi huduma bora.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib amesema kwamba mkoa huo katika kipindi hiki cha kuelekeea kilele cha kutimia miaka 61 ya mapinduzi jumla ya miradi 18 itazinduliwa na mingine kuwekewa mawe ya msingi na baadhi kufunguliwa.
Amewataka wananchi kuendelea kushirikiana katika katika uendelezaji wa miradi ya maendeleo na kwamba kwa upande wa mahakama hivi sasa inashuhudiwa kuwepo mabadiliko makubwa ya kuboresha miundo mbinu ikiwemo ujenzi wa ofisi za kisasa.
Hafla hiyo ni mfululizo wa shughuli mbali mbali zinazoendelea hivi sasa katika visiwa vya Unguja na Pemba ikiwa na shamra shamra za kutimia miaka 61 ya mapinduzi matyukufu ya Zanzibar ya Januari 64 na kilele cha sherehe hizo kitafanyika Januari 12 mwaka huu wa 2025.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo chake cha Habari leo Ijumaa Disemba 27, 2024.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake