Wednesday, December 4, 2024

MAKAMU WA RAIS AKIWASILI NCHINI ANGOLA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Angola Mhe. Balozi Téte António wakati akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Catumbela nchini Angola leo tarehe 04 Desemba 2024. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Marekani, Kongo na Zambia kuhusu Ushoroba wa Lobito (Lobito Corridor), ambapo Tanzania ni mgeni mwalikwa katika Mkutano huo unaofanyika katika mji wa Lobito nchini Angola tarehe 04 Desemba 2024.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake