Wanakijiji wa Kijiji cha Kalungu Kata ya Ivuna Wilaya ya Momba Mkoani Songwe wametakiwa kufuata taratibu za kisheria kupitia kwa Viongozi wao wa Serikali ya Kijiji ili kuepuka migogoro ya wao kwa wao au wao dhidi ya Serikali.
Kauli hiyo ilitolewa Disema 16, 2024 na Mkuu wa Kituo cha Kamsamba Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Majuto William Ntwale alipofanya Mkutano na wanakijiji hao na kuwapa elimu juu ya umuhimu na faida za kutatua migogoro ya ardhi kwa kufuata sheria ili kuepusha madhara katika jamii.
Mrakibu Ntwale alisema "Endapo mpatapo changamoto za migogoro ya ardhi basi hamna budi ya kufuata sheria na miongozo ya ardhi ili kuweza kutatua migogoro hiyo"
Pamoja na elimu hiyo Mrakibu Ntwale aliwaomba wanakijiji hao kuendelea kutoa taarifa za siri za wahalifu na Uhalifu ikiwa ni pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake