Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma, amesema Mpango mkakati jumuishi wa jinsia katika Michezo ni nyenzo muhimu ya kuleta usawa wa kijinsia katika jamii.
Akizindua mpango huo, huko katika Viwanja vya Basketball Mao - Zedong, Mhe. Riziki amesema Mpango huo utasaidia kushirikisha na kuleta usawa wa kijinsia katika Michezo.
Aidha amesema Mpango huo, utakuwa jumuishi kwa jinsia zote na hautomuacha mtu nyuma.
Hata hivyo Mhe. Riziki ametoa wito kwa Wanamichezo, Wadau wa Michezo, Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa Ujumla kuusoma na kuufahamu ili kuweza kuzingatia usalama katika Michezo.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Viajana, Utamaduni na Michezo Bi Fatma Hamad Rajab, Afisa Mdhamini katika Wizara hiyo, Mfamau Lali Mfamau amesema Mpango huo utaleta tija kwa Wanamichezo.
Aidha amesema Mpango huu pia utasaidia kuongeza ushawishi na kuondosha vikwazo katika Michezo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) Jamila Mahmoud Juma amesema lengo la mpango huo ni kukuza usawa wa kijinsia na ujumuishi kupitia michezo.
Hata hivyo amesema Mpango huo unatoa fursa sawa kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu sambamaba na kuleta mabadiliko ya usawa wa kinsia katika michezo.
Mpango Mkakati Jumuishi wa Jinsia katika Michezo Zanzibar 2024/2025-2028/29 unatekelezwa na GIZ, BMZ, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na MICHEZO na Mradi wa Kanda wa Michezo kwa Maendeleo Afrika ambapo pia umejumuisha Utambulisho wa Muongozo wa Ulinzi katika Michezo, uliotarishwa na Zafela.
No comments:
Post a Comment