Friday, December 13, 2024

PSPTB YATANGAZA MATOKEO YA MITIHANI YA 29, WAWILI WAFUTIWA MATOKEO


Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Godfred Mbanyi akizungumza wa waandishi wa habari wakati wa kutangaza matokeo ya mitihani ya 29 ya PSPTB iliyofanyika kuanzia tarehe 11 hadi 15 Novemba, 2024 katika vituo sita vya mitihani Tanzania bara na Visiwani.

Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetangaza rasmi matokeo ya mitihani ya 29 ya PSPTB iliyofanyika kuanzia tarehe 11 hadi 15 Novemba, 2024 katika vituo sita vya mitihani Tanzania bara na Visiwani.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Godfred Mbanyi amesema jumla ya watahiniwa wapatao 1,403 walisajiliwa ili kufanya mitihani hii ambapo watahiniwa 1,314 walifanya mitihani hii ambapo wengine wamekosa kufanya mitihani kutokana na sababu mbalimbali.

Mbanyi amesema kati ya watahiniwa 1,314 jumla ya watahiniwa 610 sawa na 46.4% wamefaulu mitihani yao, watahiniwa 663 sawa na 50.5% watarudia baadhi ya masomo kuanzia somo moja mpaka masomo matatu kutegemeana na masomo idadi ya masomo aliyofeli na watahiniwa 41 sawa na 3.1% wamefeli masomo yote waliyofanya katika ngazi zao.

"Bodi ya wakurugenzi imefuta matokeo ya watahiniwa wawili wa kituo cha TRITA Moshi kwa kuhusika na uvunjifu wa kanuni na taratibu za mitihani ya 29 ya Bodi na adhabu hii ya inaambatana na kutofanya mitihani ya Bodi kwa vipindi vitatu mfululizo " Alisema Mbanyi

Mbanyi Ametoa wito kwa watahiniwa wote kwa kutojihusisha na vitendo vya aina yoyote vya kudanganya wakati wa mitihani kwa kuwa wamejipanga vizuri hasa kwenye usimamizi mzuri kwani mitihani ya Bodi inafanyika katika vyumba vyenye kamera (CCTV) hivyo yoyote atakayebainika atachukuliwa hatua stahiki

Pia amesema Bodi hiyo kwa mara ya kwanza imeanza kuzaliwa wataalamu wa Wakaguzi kwenye eneo la Ununuzi na Ugavi ambapo wameanza na wataalam 61 walihudhulia mafunzo hayo na wawili hawakuweza kukidhi vigezo vya programu yao lakini 59 wamekidhi na wamefanya mtihani wao na wamefaulu kwa mujibu wa mitihani ya Bodi.

Mbanyi amewaomba waajiri wote kutambua kuwa eneo la Ununuzi na Ugavi ni nyeti na Serikali imekuwa ikipata hoja nyingi na zingine zinashindwa kujibika wakaguzi wanapokuwa eneo la ukaguzi kutokana na wengi wanaokaguliwa na wanaokagua kukosa uweledi wa namna gani taratibu za manunuzi zinapaswa kwenda.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake