Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Tanzania Mhe Mwanaidi Ali Khamis akiwa katika picha ya pamoja na Watoto wa Nyumba ya Kulelea Watoto Yatima Mazizini Unguja Wilaya ya Magharibi "B " Unguja baada ya kukwakabidhi Vyakula vilivotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe Mwanaidi Ali Khamis akikabidhi Vyakula kwa Wazee wa Nyumba ya Wazee Sebleni na Welezo, kwa ajili ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka mpya.
Na WMJJWM- Zanzibar
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe Mwanaidi Ali Khamis amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan anawajali watu wenye Mahitaji Maalum kwani ameweka mazingira mazuri ya kuwalinda na kuwapatia huduma muhimu hasa katika Makao ya Watoto na Makazi ya Wazee yaliyopo nchini.
Naibu Waziri Mwanaidi amesema hayo Zanzibar Desemba 26, 2024 wakati akitoa zawadi za Sikukuu ya Christmas na Mwaka kwa niaba ya Rais Samia katika Makao ya Watoto na Makazi ya Wazee Zanzibar.
"Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kawaida yake inapofika msimu wa Sikukuu kama hizi kutoa zawadi Kwa watoto, wazee na wananchi ili waweze kufurahia kwa pamoja, na leo ameona ni vema kuwafikia watu wa Zanzibar" amesema Naibu Waziri Mwanaidi.
Aidha Naibu Waziri Mwananidi amewataka wananchi kufurahia sikukuu za mwisho wa mwaka kwa kuwajali na wenye mahitaji Maalum ikiwa pamoja na kuwapa msaada na mahitaji mbalimbali.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake