Thursday, December 19, 2024

RAIS WA ZANZIBAR DK.HUSSEIN MWINYI AZUNGUMZA NA TUME YA MABORESHO YA KODI TANZANIA


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na Tume ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Maboresho ya Kodi, Ikulu Zanzibar iliyofika kujitambulisha.

Katika maongezi na Tume hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wake, Balozi Ombeni Sefue na ujumbe wake, Rais Dk. Mwinyi wamejadili mambo mbalimbali ikiwemo mapendekezo yatakayo zishauri Serikali mbili za SMZ na SMT kuhusu masuala ya kodi.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuiteua Tume hiyo na kueleza kuwa itasaidia kuimarisha na kubadilisha mifumo ya kodi kwa Serikali zote mbili za SMZ na SMT, itakayoleta mageuzi kwenye biashara likiwemo eneo la kodi hadi kukamilika kwake.

Kwa upande wake Balozi Sefue amezishukuru Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuahidi ushirikiano na Tume hiyo.

IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake