TANGAZO LA KISOMO NA DUA, NEW YORK
Tujumuike na Ebra NY mtoto wa mzee Nyagaly anaeishi USA, New York katika kisomo na dua siku ya JumamosiTar 21, 2024 saa 10 jioni (4pm) na baada ya kisomo Ebra NY anarajiwa kuelekea Tanzania kuungana na wana familia , ndugu, jamaa na marafiki katika maombolezo ya msiba.
Kisimo na dua kitafanyikia.
1144 Rosedale Ave,
Bronx, NY 10472
Timu ya Vijimambo blog na Vijimambo TV ilipokea taarifa ya msiba wa baba ya mwenzetu Ebra NY kwa masikitiko makubwa na timu nzima inatoa pole kwa familia kwa kufiwa na mpendwa baba yao. Kwani huu ni msiba mkubwa.
Mzee Nyagaly alifikwa na umauti siku ya Ijumaa ya tarehe 13/12, /2024 huko Nachingwea Mkoa wa Lindi. Na kupumzishwa siku ya Jumamosi ya tar 14/12 /2024 Kijijini cha Ikungu-Nachingwea, Lindi.
Mzee Nyagaly amefariki akiwa na miaka 95, ameacha mjane Bint Bakari Kanjele aliekuwa amebahatika nae kupata watoto 8, wa kike mmoja na wakiume 7.
Mzee Nyagaly ameacha watoto 8 na wajukuu 33
Inna Lillahi wa ilayhi raji'un Mzee wetu apumzike kwa amani
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake