Na John Walter -Babati
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati super brands LTD David Mulokozi amewaalika wafanyakazi wake kwenye karamu ya chakula cha jioni iliyoandaliwa kifalme na kuitwa Royal Party.
Shughuli hiyo imefanyika Mjini Babati Mkoani Manyara huku wafanyakazi hao wakivalia mavazi ya aina mbalimbali yanayoashiria ufalme.
Tofauti na sherehe zingine za kuwa na foleni za chakula, watu walikuwa wakihudumiwa kwenye meza zao vyamula na vinywaji.
Burudani ya nguvu ilishushwa na wasanii Rayvanny, Mama Mawigi, Babu wa Tiktok na Zuli Comedy.
Mkurugenzi wa Mati Super Brands Limited David Mulokozi amesema amelenga kuwapongeza wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kufanya kazi kwa weledi na ufanisi mkubwa mwaka mzima wa 2024 .
“Kampuni ya Mati Super Brands Limited iliyoanza kama mchicha na sasa imekua mbuyu ,ilianza kama mradi mdogo wa kuhudumia mikoa michache ya Tanzania lakini leo tuna wateja nchi nzima na karibia Afrika nzima, alisema Mulokozi
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda ameipongeza Kampuni ya Mati Super Brands Limited kwa kulipa kodi stahiki za serikali na kutoa fursa za ajira kwa vijana hivyo kupunguza changamoto ya ajira katika mkoa wa Manyara na Taifa.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake