Wakili wa mahakama kuu ya Tanganyika Deogratius Mahinyila leo ametangazwa kuwa mwenyekiti mpya wa taifa wa Baraza la Vijana wa CHADEMA yaani BAVICHA kufuatia uchaguzi mkuu wa baraza la vijana wa CHADEMA uliofanyika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam
Wakili Deogratius Mahinyila ni mhitimu wa chuo kikuu University of Dar es Salaam (UDSM) degree LLB na amepita shule ya Sheria na kusajiliwa pia kuthibitishwa kutumika na wateja wa huduma za kisheria na utetezi kama wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania
Wakili Deogratius Mahinyila anarithi mikoba ya mwalimu John Pambalu ambao muda wake wa uongozi kama mwenyekiti wa BAVICHA taifa umekwisha
Wakili Deogratius Mahinyila amepitia mengi ambayo wanasiasa wa upinzani hutegemea kuyapitia katika siasa za Tanzania ambazo zimetawali kwa wivu uliopitiliza na chama dola kongwe CCM kinachofanya kila kiwezekanavyo kubaki madarakani hata kwa mbinu zisizo za kidemokrasia, utawala bora na mikakati mingine haramu ambayo kisheria haikubaliki kwa kufuatana na katiba ya nchi tuliyo nayo..
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake