Monday, January 13, 2025

WALIOKAIDI UKAGUZI MAGARI YA SHULE WAKAMATWA, WANANCHI WAOMBWA KULINDA KUNDI JIPYA LA WATUMIAJI WA BARABARA.

Na. Mwandishi Jeshi la Polisi Arusha.
Jeshi la Polisi kikosi cha usalama Barabarani kimesema kuwa baada ya kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa magari ya shule(School Bus) kwa kipindi cha likizo ambacho kilitangazwa ili kuondoa usumbufu kwa wanafunzi wanaotumia vyombo hivyo kimeanza kuwakamata wale wote walio kaidi agizo hilo huku kikosi hicho kikiwaomba wananchi kuweka uangalizi wa kundi hilo.

Akiongea katika zoezi hilo Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed amesema kuwa kikosi hicho kilitangaza zoezi hilo ambapo ameweka wazi kuwa wameanza operesheni za ukamataji wa magari ambayo haya jakaguliwa na kikosi hicho.
Ameongeza kuwa takwimu zinaonyesha kuna zaidi ya magari 563 ambayo yanatoa huduma kwa wanafunzi ambapo baada ya ukaguzi huo inaonesha bado magari 178 huku akiweka bayana kuwa kuanzia leo Januari 13,2025 wameanza kuwamata madereva waliokaidi ukaguzi huo.

SSP Zauda akatumia fursa hiyo kuwataka wamiliki na madereva kupeleka magari yao katika kikosi cha usalama barabarani ili kufanya ukaguzi na kuweka mazingira salama ya watumiaji wa vyombo hivyo ambao ni wanafunzi huku akisisitiza kuwa watakaoendelea kukaidi watachukuliwa hatua za kisheria.
Sambamba na hilo akasema kuwa kikosi hicho kinatambua kuwa kuna kundi jipya la watumiaji wa Barabara ambao ni wanafunzi wa shule za awali walioanza shule mwaka huu ambapo amewaomba wananchi kushirikiana na Jeshi hilo katika kuwaelekeza matumizi sahihi ya Barabara na kundi hilo kuwa na wasimamizi kipindi cha Kwenda na kurudi majumbani.

Pia akatoa wito kwa madereva kutambua kuwa kuna kundi jipya la watumiaji wa Barabara akiwataka kuchukua tahadhari na kufuata sheria za usalama barabarani ili kundi hilo liendelee kuwa salama kipindi chote.


No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake