Tuesday, February 11, 2025

AFUKUZWA CCM KWA KUPINGA UAMUZI WA MKUTANO MKUU WA CCM TAIFA



Mchungaji Godfrey Malisa amefukuzwa uanachama na Chama cha Mapinduzi (CCM), Februari 10, 2025 kwa tuhuma za kukiuka Katiba na maadili ya Chama hicho.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Merce Mollel amesema uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa

Aidha, hatua ya kufukuzwa kwa Malisa imeelezwa kuwa imetokana na kauli alizokuwa akizitoa kupinga uamuzi wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wa Januari 19, 2025 akidai kupitishwa kwa Rais Samia Suluhu na Dkt. Hussein Mwinyi (Zanzibar) kuwania Urais wakiwa Wagombea pekee wa chama kumekiuka Katiba ya CCM

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake